FLOYD Mayweather, bondia anayeongoza kwa kulipwa fedha nyingi dunia, amesema atalipa gharama zote zitazohitajika katika msiba wa George Floyd. Inaripoti mtanzano wa BBC…(endelea).
Floyd, mmarekani mweusi aliuawa wiki iliyopita akiwa chini ya polisi wa Minneapolis. Kifo chake kimesababisha maandamano katika miji zaidi 80 nchini humo huku mauaji, uharibifu na uporaji vikishuhudiwa.
Taarifa za Mayweather kugharamia msiba wa Floyd zimethibitishwa na Leonard Ellerbe, Mtendaji Mkuu wake.
“Alionekana kama amechanganyikiwa kutokana na habari za kifo hicho, ni kweli ameahidi kulipa gharama zote za msiba wa Floyd,” amesema Ellerbe alipozungumza na mtandao wa ESPN.
Katika hatua nyingine, Umoja wa Ulaya (EU), umemuonya Donald Trump baada ya kauli yake kwamba, atatumia jeshi kukabiliana na ghasia.
EU imeeleza kwamba, hatua hiyo inaweza kuzidisha machafuko na kuwa na matokeo mabaya zaidi kuliko inavyotarajiwa.
Trump mapema leo mapema kwamba, iwapo magavana na mameya watashindwa kurejesha Amani kwenye maeneo yao, atalazimika kutumia jeshi.
“EU imeshtushwa na aina ya kifo cha Floyd, tena chini ya vikosi vya usalama. Haya ni matumizi mabaya ya madaraka,” amesema Josep Borrell, mkuu wa masuala ya kigeni na kuongeza “matumizi ya jeshi yanaweza kuwa na madhara zaidi.”
Leave a comment