May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mayele aibeba Yanga mbele ya Geita Gold

Spread the love

MFUMANIA nyavu wa Yanga Sc. Fiston Mayele anaweza kuweka rekodi ya kuwa mfungaji aliyefunga goli mapema zaidi ikiwa ni sekunde ya 50 tangu mchezo kuanza kati ya timu yake na Geita Gold FC. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Katika mchezo huo uliopigwa leo tarehe 6 Machi, 2022 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Geita ilihamishia mchezo huo katika dimba hilo badala ya Nyankumbu ili kuongeza kipato.

Aidha, goli hilo pekee la Mayele ndilo lililoipa pointi tatu Yanga na kuendelea kujichimbia kilele mwa Ligi kwa kufikisha pointi 45.

Yanga ambayo imeendeleza rekodi ya kushinda mechi zote za ugenini, licha ya kuwakosa wachezaji wake watano muhimu wa kikosi cha kwanza waliocheza mechi iliyopita na Kagera Sugar, leo imezidisha pengo la pointi kati yake na mpinzani wake mkubwa Simba Sc. Wenye pionti 34 na mchezo mmoja mkononi.

Baadhi ya wachezaji hao waliokosekana leo ni Khalid Aucho, Saidoo Ntibazonkiza, Shaban Djuma na Farid Mussa ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Nafasi zao zimezibwa na Dickson Job, Paulo Godfrey, Feisal Slaum, Yasin Mustapha na Deus Kaseke.

Aidha, Mayele ambaye sasa amefikisha magoli 10, alipachika bao hilo mapema kutokana na safu ya ulinzi ya Geita Gold kushindwa kuwa na utulivu.

Bao hilo la Mayele ambaye ni mshambuliaji namba moja wa Yanga anakuwa sawa na Lusajo Mwaikenda ambaye anakipiga katika klabu ya Namungo FC.

Aidha, kesho tarehe 7 Machi, 2022 Simba watajiuliza mbele ya Dodoma FC katika mchezo ambao utapigwa katika dimba la Benjamini Mkapa.

error: Content is protected !!