January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mawaziri wanawake Tanzania wafikia 9

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya

Spread the love

 

 

IDADI ya wanawake katika baraza jipya la mwaziri nchini Tanzania litakaloapishwa leo Jumatatu, tarehe 10 Januari 2022, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan imeongezeka na kufikia tisa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Baraza hilo jipya la mawaziri 25, limeshuhudia idadi ya wanawake ikiendelea kuongezeka kutoka saba hadi tisa huku naibu mawaziri ikipungua kutoka sita hadi watano kati ya 26.

Ingizo jipya la mawaziri ni Dk. Pindi Chana anayekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu pamoja na Angelina Mabula aliyepanda kutoka naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kuwa waziri kamili.

Wengine na wizara zao kwenye mabano; ni Jenista Mhagama (Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora), Ummy Mwalimu (Afya) na Profesa Joyce Ndalichako, (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, Jenista Mhagama

Pia, wamo Dk. Dorothy Gwajima (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye mahitaji maalum), Dk. Ashatu Kijaji (uwekezaji, viwanda na biashara), Dk. Stegomena Tax, (Ulinzi) na Balozi Liberata Mulamula, (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Naibu waziri wamebaki walewale huku wakipungua baada ya Angelina kupanda kuwa waziri kamili kuchukua nafasi ya Wilium Lukuvu ambaye ametoswa. Nafasi ya Angelina kwenye wizara hiyo ya ardhi ameteuliwa Ridhiwani Kikwete.

Waliobaki na wizara zao kwenye mabano ni, Ummy Nderiananga, (Sera, Bunge na Uratibu), Mary Masanja (maliasili na utalii), Mwanaidi Khamis (maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum), Maryprisca Mahundi (maji) na Pauline Gekul (utamaduni, sanaa na michezo).

error: Content is protected !!