
Maporomoko ya mto Nile
MAWAZIRI wanaohusika na masuala ya Maji katika nchi za Bonde la Mto Nile, wanatarajia kukutana 4 Juni mwaka huu, nchini Tanzania kwa ajili ya mkutano wa 23 wa mwaka. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kwa mujibu wa Afisa habari wa Wizara ya Maji, Dennis Kiilu, ushirikiano wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative – NBI) ni utaratibu wa ushirikiano wa kiserikali wa kikanda baina ya nchi wanachama 10 ambazo ni sehemu ya bonde hilo.
Kiilu amesema nchi hizo ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.
Amefafanua kuwa nchi ya Eritrea inashiriki kama mtazamaji, na kwamba ushirikiano huo ulizinduliwa jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari 1999 kwa lengo la kuwa na utaratibu maalum wa kusimamia kwa pamoja na kuendeleza rasilimali za maji katika Bonde la Mto Nile.
Ameeleza kuwa ushirikiano huu pia una faida kubwa za kijamii, kiuchumi na kukuza amani na usalama wa kikanda ambao unaongozwa na dira ya pamoja ambayo ni: kutoa haki sawa ya matumizi ya maji ya Mto Nile kwa nchi wanachama kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.
More Stories
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN
Watuhumiwa 5 ujambazi wauawa Dar, bastola…
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco