July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mawaziri kujadili umeme A. Mashariki

Spread the love

UJUMBE wa mawaziri na viongozi wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki, wameahidi kuunga mkono harakati za kutafutia muafaka tatizo la upungufu wa nishati. 

Viongozi kadhaa wakiwemo mawaziri na makatibu wakuu wa wizara watasaidiwa na viongozi wenye usemi katika sekta binafsi ya nishati katika kikao cha Nishati Afrika Mashariki kitakachofanyika Machi 25-27 jijini Nairobi kuangalia dharura ya mgogoro wa kusambaza nishati.

Baadhi yao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya, Joseph Njoroge, Waziri wa Nishati na Madini wa Zambia, Christopher Yaluma Waziri wa Miundo Msingi wa Rwanda, James Musoni na Maria Kiwanuka ambaye ni Mshauri Mkuu wa Rais na afisa katika ofisi ya Wizara ya Fedha nchini Uganda.

Wazungumzaji muhimu kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), IFC, Barclays, Symbion Power, KenGen, KPLC, UMEME na EEP watazungumza kuhusu hatua zinazoweza kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati.

Hatua hizo ni pamoja na; nafasi muhimu ya usambazaji umeme katika mchakato wa kuendeleza viwanda, umuhimu wa nishati, jinsi ya kukabiliana na vizuizi vya mikopo na jinsi gharama ya mikopo katika kanda inaweza kupunguzwa kwa kuimarisha usambazaji umeme.

Meneja wa Mpango wa EnergyNet, Veronica Bolton-Smith amesema kuwa mawaziri hao wamekubali mialiko; hasa ikizingatiwa kwamba mkutano huu unalenga washirika wachache.

Amesema kuwa, uwepo wa vigogo wanne katika sekta binafsi ya nishati katika kanda hii ni ishara ya haja ya kuwa na mdahalo wenye lengo.

error: Content is protected !!