Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawasiliano ya barabara Dar mikoani yarejea
Habari Mchanganyiko

Mawasiliano ya barabara Dar mikoani yarejea

Spread the love

MAWASILIANO ya barabara kati ya jiji la Dar es Salaam na mikoani imerejea leo baada ya magari kuanza kupita katika daraja la Kiluvya ambalo jana lilikuwa limejaa maji na hivyo kufungwa kwa ajili ya usalama, anaandika Richard Makore.

Leo mtandao huu wa MwanaHALISI Online umeshuhudia mabasi yaendayo mikoani yakipita katika daraja hilo baada ya vyombo vya ulinzi na usalama kujiridhisha kwamba hakuna madhara yanayoweza kutokea hapo tena.

Jana vyombo hivyo viliyazuia magari yote kupita hapo na hivyo kuelekeza mabasi yaliyokuwa yakitokea mikoa mbalimbali ya bara kupita Bagamoyo ili kuingia jijini Dar es Salaam.

Mvua zilizonyesha juzi na jana mchana zilileta madhara baada ya daraja la Kiluvya linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kuja maji na hivyo magari kushindwa kupita.

Kutokana na daraja hilo kujaa maji hudumza za usafiri wa magari ya abiria, mizigo na binafsi ulisitishwa na wananchi wakaombwa kutumia barabara ya Bagamoyo.

Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ya Kaskazini, Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Magharibu.

Aidha, mvua hizo zilisababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kujaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!