August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mawakili wavutana kesi ya ‘Wahujumu’ uchumi

Spread the love

KESI ya kuhujumu uchumi inayomkabili Mohammedi Mustafa na mwenzake Sammuel Lema imeendelea tena jijini Dar es Salaam katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu huku mawakili wa upande wa mashitaka na utetezi wakivutana vilivyo, anandika Faki Sosi.

Awali watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani juzi katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa 222.

huku upande wa utetezi ukipinga shitaka la 221 la utakatishaji fedha linalowakabili wateja wao.
Alex Mgongolwa Wakili anayeongoza jopo la Mawakili wa upande wa utetezi alidai kuwa shitaka hilo halina mashiko kisheria huku upande wa Mashtaka ulioimba Mahakama hiyo muda wa kujibu hoja hizo.

Katika siku ya leo, upande wa mashitaka umedai kuwa hoja za upande utetezi zimegemea kwenye kifungu cha 13 pekee cha sheria ambazo kifungu cha 12 (a), (b), (c), (d), na (e) kinaainisha makosa hayo.

Kishenyi Mutalemwa Wakili wa serikali amedai kuwa chini ya kifungu Namba 12 (a) kila kosa lazima liwe na dhana ambapo kushiriki kwenye mali ambayo inatokana na uhalifu ni miongoni mwa ushiriki wa kosa hilo.

Oswadi Tibabyekonya wakili mkuu wa serikali amesema hoja ya kupinga shitaka la 221 kwamba sio kweli kuwa shitaka hilo lina dosari kwani limeweka wazi kuwa washitakiwa walifanya muamala wa kusafirisha Sh. 420 Millioni huku wakijua fedha hizo zinatokana na kughushi na kukwepa kodi .

Mvutano baina ya mawakili wa pande hizo mbili uliendelea ambapo Alex Mgongolwa wakili wa upande wa utetezi amedai kuwa viini vyote vya kosa hilo vimeaanishwa kwenye kifungu cha 12 na kwamba tafsiri inayotolewa katika kipengele cha ya tatu cha kosa hilo.

Ambapo amedai kuwa katika kifungu hicho cha tatu cha sheria ya utakatishaji fedha kosa la utakatishaji fedha limetajwa katika hatua tatu ambazo ili liwe kosa lazima mtendaji apitie hatua hizo.
na kwamba kifungu Na. 12 hakitoi tafsiri ya kosa hilo.

Amedai kuwa sio kila matendo ya wizi ni utakatishaji fedha ambapo kitendo cha kuficha uhalisia wa fedha hizo ndio chanzo cha utakatishaji fedha na kwamba shitaka hilo lifutwe.

Hakimu Wilbard Mashauri baada ya kusilikiliza hoja za pande zote mbili amesema kuwa atalitolea maamuzi shauri hilo tarehe 10 Agosti mwaka huu.

error: Content is protected !!