Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mawakili wa utetezi wamhoji shahidi kuhusu simu za akina-Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Mawakili wa utetezi wamhoji shahidi kuhusu simu za akina-Mbowe

Spread the love

 

UPANDE wa utetezi, katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, wamemhoji Mchunguzi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Jeshi la Polisi, Inspekta Innocent Ndowo, juu ya taarifa alizozinyonya katika simu zinazodaiwa kuwa za baadhi ya washtakiwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Inspekta Ndowo alihojiwa maswali na mawakili wa utetezi, kuanzia jana Jumanne hadi leo Jumatano, tarehe 19 Januari 2022, baada ya kuwasilisha taarifa hizo katika Mahakama Kuu,  Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Taarifa hizo zilizowasilishwa mahakamani hapo na Inspekta Ndowo, ni ujumbe mfupi wa maneno (meseji), katika mitandao ya kijamii ya Telegram na WhatsApp, zinazodaiwa kufanywa na Mbowe na mshtakiwa mwenzake, Mohammed Abdillah Ling’wenya, kwenda kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Denis Urio.

Mbali na Mbowe na Ling’wenya, washtakuwa wengine katika kesi hiyo namba 16/2021, yenye mashtaka sita ya ugaidi ni, waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan na Adam Kasekwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizowasilishwa mahakamani, Mbowe anadaiwa kuwasiliana na Urio kati ya Julai hadi Agosti 2020, ambapo mazungumzo yao yalionesha namna mwanasiasa huyo alivyomuomba amtafutie vijana wa kumfanyia kazi.

Wakili Nashon Nkungu, alimuuliza Inspekta Ndowo kama uchunguzi aliofanya kuhusu vielelezo hivyo unahusiana na mashtaka yaliyoko mahakamani hapo kama ifuatavyo;

Nkungu: Analysis nani aliifanya?

Shahidi: Mimi

Nkungu: Baada ya analysis yako ukaagundua meseji hizi na mazungumzo haya ni relevant kwa makosa haya?

Shahidi: Hapana, ni relevant kwa namna ambavyo nimeombwa

Nkungu: Tuambie ombi lako unalofanyia kazi?

Shahidi: Kufanya uchunguzi wa mawasiliano na miamala ya fedha.

Nkungu: Kwa hiyo kwa ushahidi wako hizo meseji ulizoleta sio relevant kwa mashtaka yaliyopo mahakamani?

Shahidi: Sijui kama ni relevance lakini nilizijibu kulingana na nilivyoombwa

Nkungu: Kwamba umeletewa uchunguze,  haujui uchunguze nini?

Shahidi: Ndiyo

Nkungu: Wewe katika moja ya taaluma zako nilisikia una utaalamu wa terrorism na crime investigation?

Shahidi: Sahihi

Nkungu: Una uelewa wa terrorism?

Shahidi: Nimesema katika uchunguzi nina uelewa

Nkungu: Kwa kuwa ulikuwa trained kwenye masuala ya uchunguzi, at least unafahamu ingredient za ugaidi?

Shahidi: Katika uchunguzi nafahamu, lakini upelelezi sifahamu

Nkungu: Katika uchunguzi wako na hasa tukichukulia wewe mtaalamu, uligundua hiki ambacho umekiextract kinahusiana na ugaidi?

Shahidi: Hilo swali siwezi kulijibu, kwa sababu anayeweza kulijibu ni yule aliyeleta  maombi ya uchunguzi

Naye Wakili John Mallya alimhoji kama ifuatavyo;

Mallya: Kwenye finding zako shahidi kwenye vielelezo umekuta taarifa zinazohusika na kesi hii, vielelezo vipi ulikuta majibu positive (chanya)?

Shahidi: Kielelezo kuanzia E F G H

Mallya: Nauliza ulikuta positive research katika uakguzi wako?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unasema kuna baadhi ya simu hukukuta taarifa ambazo uliulizwa kwayo,  si ndiyo zile umezipa majina A B C D?

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Unafahamu simu ni person property ya mtu, ni mali ya mtu unaelewa hilo jambo?

Shahidi: Ndio

Mallya: Umechunguza, umekuta haina chochote kuhusiana na kesi, ni sahihi umrudishie mmiliki au unakaa nayo?

Shahidi: Unaongelea kwamba mimi natakiwa kumrudishia huyo aliyemkamata? Sijajua kama ni sahihi

Mallya: Nimemshuku bwana fulani ana simu inayohusika na mambo ya wizi, nikagundua nimekosea, nimrudishie mali yake ni sahihi?

Shahidi: Sijakuelewa

Mallya: Hii mali ya mtu, Askari alishuku ina wizi ndani yake, ameenda kuichunguza kwa mchunguzi kama wewe, ukasema unacho-suspect humu hamna, yule mtu ukamrudishia au mpelelezi wake?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Ulivyoulizwa kwenye item A B C D hakuna hiyo report  inayoonesha majibu negative (hasi)?

Shahidi: Sikuona sababu ilikuwa inahitajika content, kwa kuwa haikuwepo hakukuwa na haja ya kuileta

Mallya: Position ya Bwire ni kwamba, hayo mawasiliano yalikuwepo, na yanaikana ripoti yako, ili tujue hayakuwepo ungeleta negative result, akitaka negative result ya uchunguzi wako ataipataje?

Shahidi: Nilipewa terms of request, ripoti yangu ilitakiwa ijikite kwenye term nilizoombwa, maana yake taarifa zile nisingeweza kuzi-include.

Shahidi hiyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!