Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mawakili wa Mbowe wasimamisha kesi
Habari za SiasaTangulizi

Mawakili wa Mbowe wasimamisha kesi

Spread the love

 

JAJI Mustapha Siyai, anayesikiliza kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameiahirisha kwa muda. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo namba 16/2021 ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inasikilizwa Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano, Dar es Salaam.

Mbali na Mbowe wengine; ni Halfani Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa leo Jumatano, tarehe 15 Septemba 2021, kwa shahidi wa pili wa Jamhuri, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni (RPC), Ramadhan Kingai kutoa ushahidi wake.

Wakatik RPC Kingai akiendelea kutoa ushahidi wake, umeibuka mvutano wa kisheria kati ya mawakili upande wa serikali na wale wa utetezi ukiongozwa na Peter Kibatala.

Mvutano huo, umetokana na upande wa utetezi kukataa maelezo ya mshatakiwa Adam Kasekwa, kwamba yalichukuliwa zaidi ya saa nne tangu alipokamatwa.

Kibatala amesema, maelezo yalichukuliwa baada ya mshitakiwa Adam kusetwa hivyo, kuomba kusikilizwa kwa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa, akitoa hoja kadhaa.

Kwanza, amesema maelezo yamechukuliwa nje ya muda wa kisheria kama ilivyoelekezwa na kifungu cha 50 (1) (a na b) cha sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 2019 na kifungu cha 51 (2).

“Maelezo yamechukuliwa zaidi ya masaa manne kutoka kwa mshitakiwa alipokamatwa na kwamba hilo ni moja ya kasoro kubwa kisheria,” amesema Kibatala

Pili, amesema kabla na maelezo yanachukuliwa kwa mshitakiwa Adam aliteswa na shahidi na zoezi hilo lilisimamishwa na yeye na wenzake.

“Tunaomba mahakama ikubaliane na maelezo yetu na kwa hoja ya pili, tunaomba kufanya kesi ndogo kwa kesi kubwa,” amesema

Akiongezea hoja, Wakili Jeremiah Mtobesya amesema,ukisoma kifungu cha 151, kinaruhusu kuondoa muda pale mtuhumiwa anakuwa anaendelea na upelelezi, lakini kwa ushaidi wa shaidi wa kwanza aliwakamata tarehe 05 na waliwaweka Rock up tarehe 06.

Amesema, mheshimiwa Jaji kuna muda hapa haujaelezewa, ukisoma ushaidi wa shahidi kwanza anasema hawa watu walihifadhiwa majira ya saa 4 ussiku.

Ameendelea kusema, ukiangalia sioni sababu kuna nini kiliwazuia wasichukue maelezo labda kama pangekuwa na ushahidi mbele yako yanayoonesha pana sababu iliyosababisha wasichukue maelezo.

“Ukisoma hukumu mbalimbalimbali za Mahakama Kuu, zinaeleza kuwa labda kama palikuwa na mazingira yakiyopeleka msichukue maelezo wakati wanafanya maelezo.”

“Jaji unaona inahitaji kesi ndogo ndani ya kesi hii kama Wakili Kibatala alivyosema kwa Kifungu cha 169 cha CPA,” amesema.

Baada ya maelezo hayo, Jaji Siyani amekubaliana na hoja ya Kibatala na Mtobesya hivyo ameahirisha kesi hadi saa 8:00 mchana ili kusikiliza kesi ndogo ya kuchukuliwa maelezo nje ya wakati pamoja na kuchukuliwa maelezo baada ya kuteswa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!