Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mawakala wa elimu watoa ufafanuzi wa udhamini
Elimu

Mawakala wa elimu watoa ufafanuzi wa udhamini

Chuo cha Qingdao kilichopo nchini China
Spread the love

KAMPUNI ya Mawakala wa Elimu Solution Ltd, imetoa ufafanuzi jinsi wanavyo wadhamini wanafunzi wa vyuo vikuu, wajasiliamali, na wafanyakazi kwenda kusoma nchini China, Japan na Kusini Korea na wanavyonufaika katika kuendesha kazi hiyo. Anaripoti Angel Willium … (endelea).

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Neithan Swed ametoa ufafanuzi huo wakati wa uzinduzi wa tovuti ya kisasa, ufunguzi wa muhula mpya wa masomo kwa mfumo wa udhamini kwa ngazi ya astashahada na mafunzo ya lugha kwa wanafunzi watakaopata nafasi.

Swed amesema wanafunzi wa vyuo wanaokwenda kusoma nchi mbalimbali wakiwemo wa ngazi ya cheti na mastazi wanaokaa nchini huko kwa miaka zaidi miwili hadi mitatu na maombi yao ufanyika mwezi Januari hadi Machi ambao ufadhili wao unakuwa kamili.

“Wanafunzi wa mastazi wanaweza kulipwa mishahara 300,000 hadi 2,000,000 na watu wa bachela wanakuwa na udhamini mdogo inaweza kuwa akalipiwa chumba cha kulala, ada akalipa mwenyewe akiwa nchini huko, au suala la nauli analipa mwenyewe na ada tunamlipia,” amesema Swed.

Aidha amesema, asilimia 10 au 20 analipa mwanafunzi na 80 inalipa kampuni, kupitia kazi hii wazazi wengi hupeleka watoto kwenda kusoma nje ya nchi na kufikia malengo na upande wa wafanyakazi watakuwa wanaenda kuongeza ujuzi katika kazi zao, hivyo ni mwezi mmoja wanaokaa nchini humo kutokana na ruhusa wanazopata katika maofisi wanayofanyia kazi.

Pia amesema, kuhusu kunufaika na kazi hiyo ni kupitia Taasisi wanazoshirikiana nazo za nje ya nchi kama China, hao ndiyo uwasaidia fedha kama mawakala.

Mawakala wa Elimu ya Solution, wamekuwa na urafiki na vyuo zaidi ya 300 kutoka nchi ya China, Japani na Korea Kusini na wamepata nafasi 1500 za masomo kwa kila muhula mpya na ngazi zote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Spread the love  SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es...

error: Content is protected !!