Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mawakala Odinga, Ruto wachelewesha matokeo, Chebukati atishia kuwatimua
KimataifaTangulizi

Mawakala Odinga, Ruto wachelewesha matokeo, Chebukati atishia kuwatimua

Spread the love

KUCHELEWESHWA kutangazwa kwa matokeo ya urais kumezidi kuzua wasiwasi nchini Kenya huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ikilaumu mawakala wa Naibu Rais, William Ruto na mpinzani wake mkuu Raila Odinga. Inaripoti mitandao ya kimataifa… (endelea)

Hadi kufikia jana jioni tarehe 12 Agosti, 2022  matokeo kutoka  maeneo viti vya wabunge 20 kati ya 290 ndiyo yalikuwa yamethibitishwa na kutangazwa rasmi na Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Webuye Mashariki, Aldai, Ndia, Nandi Hills, Kaiti, Moiben, Ainabkoi, Yatta, Gatundu South, Gilgil, Lamu Mashariki, Kangundo, Ol Jorok, Kathiani, Baringo ya Kati, Kipkelion Mashariki na Mwingi Kaskazini.

Maeneo 50 ya uchaguzi yalikuwa yamefika kituo cha majumuisho Bomas, hilo likimaanisha kuwa matokeo kutoka maeneo zaidi ya 240 ya viti vya ubunge bado hayajafikishwa.

Aidha, Chebukati alisema kusuasua kwa matoke ohayo kunasababishwa na tabia ya mawakala Dk. Ruto na Odinga kuwasumbua maofisa wa IEBC wanaojumlisha matokeo.

Alitishia kuwatimua mawakala wa Dk. Ruto na Odinga kutoka ukumbi wa Bomas iwapo wataendelea kuwasumbua maofisa hao.

Pia aliwataka mawakala hao washauriane naye iwapo kuna utata au suala lolote kuhusu matokeo haya badala ya kuzingira maofisa wa tume wanaojituma usiku na mchana kuhakikisha shughuli hiyo inakamilika.

“Fuatilia mchakato huu na stakabadhi ambazo zipo lakini msigeuke wakaguzi. Nakili dosari yoyote kisha utume ripoti. Iwapo kuna tatizo lolote, basi mlete kwangu binafsi ili nilishughulikie,” alisema Chebukati.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, IEBC itaharakisha mchakato wa kuthibitisha kura hizo ilimradi mawakal hao hawatoendelea kuwasumbua wafanyakazi wa IEBC.

Katiba ya Kenya inaipa tume hiyo siku saba kutangaza matokeo ya Urais ambazo zinatamatika wiki ijayo Jumanne.

“Naamrisha kuwa kila hatua ya kukagua na kuhakiki matokeo ichukue dakika 15 kwa kila ofisa wa uchaguzi. Pia, tutaongeza wafanyakazi zaidi kuimarisha kasi ya kuthibitisha kura,” aliongeza.

Kamishina wa IEBC, Abdi Guliye kwenye kikao kingine, aliwakoromea mawakala wa Dk. Ruto na Odinga na kusema iwapo tatizo hilo litaendelea, basi wataongeza maofisa wa usalama na kuwatimua mawakala hao.

“Tuna usalama wa kutosha, hasa katika sehemu ya ukumbi ambapo fomu zinahakikiwa. Nawaomba wote wawe na heshima kwa wafanyakazi wa IEBC,” akasema Guliye.

MTANDAO HAUJADUKULIWA

Ofisa Mkuu Mtendaji, Hussein Marjan naye alikanusha taarifa kuwa mtandao wa IEBC ulikuwa umedukuliwa na kusema wameweka usalama wa hali ya juu kiteknolojia kwenye vifaa wanavyovitumia.

“Kuna habari feki ambazo zinaenea sana kuwa mtandao wetu ulidukuliwa, hilo si kweli,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!