March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mawakala Chadema, NCCR wasulubiwa Ukonga

Spread the love

MSIMAMIZI wa kituo cha Uchaguzi Pugu mnadani, Mustapha Zayumba amewatimua mawakala Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mustapha amesema, amewatimua mawakala hao kwa madai ya kutokuwa na barua za mtendaji wa kata.

Mawakala wa Chadema wamelalamika kwamba, katika viapo waliyopewa vya kusimamia uchaguzi, walielezwa kuwa fomu zote watazikuta kituoni.

“Nashangaa eti hapa wanatuambia haturuhusiwi kusimamia mpaka tuwe na viapo na barua za mtendaji jambo ambalo awali hawakueleza mahitaji hayo,” alilalamika wakala mmoja na kuongeza:

“Tumekwenda kwa mtendaji hatujamkuta hivyo tunaonekana hatuna sifa.”

Msimamizi Mustapha amesema, hata mawakala wa CCM nao walitimuliwa na kwamba, wamekwenda kufuata barua hizo.

Amesema “hakuna wakala yoyote anayependelewa ila utaratibu lazima ufuatwe.”

error: Content is protected !!