Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mavunde alia na siasa chafu
Habari za Siasa

Mavunde alia na siasa chafu

Spread the love

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, amewataka wanasiasa kuachana na siasa zenye viashiria vya uvunjifu wa amani. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Alitoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Dodoma mjini juu ya mkakati wa kujiendeleza kuuchumi kilichofanyika jijini Dodoma .

Mavunde amesema kuwa kuna haja kubwa ya wanasiasa kujiepusha na siasa zenye chuki badala yake siasa zijengwe kwa misingi ya kujenga hoja kwa lengo la ushindani na kulinda amani ya nchi.

Aidha amewataka akina mama hao kuhakikisha wanatimia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwa lengo ya kujipatia maendeleo kwa wao wenyewe na jamii kwa ujumla wake.

Akiendele kuzungumza na akina mama hao aliwataka kuwa baraza la mfano na kujitokeza zaidi kuwasaidia akina mama wenzao, kisiasa, kihuchumi na kijamii ili kuwafikia walengwa bila kuwa na ubaguzi.

Katika hatua nyingine Mavunde amewataka viongozi ndani ya chama kuwa wabunifu na kubuni miradi mbalimbali ambayo itawawezesha kujikwamua kiuchumi badala ya kusubiria misahada kutoka kwa wafadhili.

Mbali na hilo amewataka akina mama wa UWT kuunda vikundi vilivyosajiliwa ili kuwezesha wataalamu watakaopita katika vikundi hivyo ndani ya kila kata kutoa elimu kwa wepesi zaidi juu ya ujasiriamali.

Kutokana na umuhimu wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi serikali inakusudia kutumia kiasi cha sh.bilioni 77 kwa ajili ya kutengeneza mandhari ya mji wa Dodoma ili kuwavutia wawekezaji na wageni wanaoingia mjini.

Alivitaja vivutio hivyo,siko la kimataifa la kisasa eneo la Nzuguni ambalo litakuwa kubwa na zuri kuliko yote Barani Afrika, stendi ya kuegesha magari yaendayo mikoani ambayo itakuwa kubwa nay a kisasa Barani Afrika yenye uwezo wa kuegesha magari ya abiria 600 kwa wakati mmoja,ujenzi wa bustani ya kupumzikia nay a kisasa itakayojengwa eneo la jacana.

Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma Mjini, Robert Mwinje aliwahasa wanasiasa hususani wa UWT kushikamana na kudumisha upendo kwa kutambua kuwa hakuna mwanachama ambaye ni maarufu zaidi ya chama.

Aidha aliwataka kutumia nafasi zao vizuri hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka kesho, na kuwataka kutowapigia debe wagombea ambao hawana sifa ya kugombea.

Alisema kuwa ikitokea kuwa wapo viongozi ambao wataonekana kuwapigia debe wagombea ambao hawana sifa ya kugombea na kuachwa wale wenye sifa kamwe hawatapitishwa kwa ajili ya kugombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!