July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mauzo ya figo yaongezeka mtandaoni

Spread the love

 

HOSPITALI kuu ya umma kutoka nchini Kenya, imeripoti kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaoulizia nakujitolea kuuza figo zao. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea)

Katika chapisho la Facebook kutoka Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, imetipoti kuwa ‘’Figo yangu ni pesa ngapi?’’ hilo ni swali lililoulizwa zaidi kupitia ujumbe kwenye ukurasa wao.

Hata hivyo hospitali hiyo ilishauri kwamba viungo vya mwili vinaweza kutolewa kwa wagonjwa tuna kusisitiza kuwa “tafadhali kumbuka uuzaji wa viungo ni marufuku na ni kinyume cha sheria, unaweza kuchangia kwa hiari yako,” ilisema.

Bango la hospitali hiyo, linaangazia hatua za kukata tamaa ambazo watu wanafikiria huku kukiwa na ongezeko la bei ya chakula na mafuta.

Aidha benki ya dunia, mapema mwezi huu imeonya kuwa Afrika mashariki ni miongono mwa maeneo yanayokabiliwa na mdororo mkubwa wa uchumi kwa sababu ya vita vya Urusi nchini Ukraine.

error: Content is protected !!