Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Mauya achukua nafasi ya Mzamiru Stars, apaa kwenda Benin
Michezo

Mauya achukua nafasi ya Mzamiru Stars, apaa kwenda Benin

Spread the love

KIUNGO mkabaji wa klabu ya Yanga, Zawadi Mauya amejmuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichosafiri kuelekea Benin mara baada ya kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin ambaye hatokuwa sehemu ya mchezo huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa kundi J, utapigwa Jumapili Oktoba 10, 2021 nchini Benin, huku Taifa Stars ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye mchezo wa jana kwa bao 1-0.

Mauya ambaye hapo awali hakuitwa kwenye kikosi hiko ambacho kiliingia kambini Oktoba 3, 2021 kujiandaa na michezo miwili dhidi ya Benin, ameenda kuchukua nafasi ya Mzamiru ambaye amesalia nchini mara baada ya mchezo wa jana kupata kadi ya njano ambayo ilitimiza idadi ya kadi tatu na kufanya kukosa mchezo ujao.

Mchezaji huyo aliunguna na wenzake siku ya jana na leo tarehe 9 Oktoba, wameanza safari kuelekea nchini Benin kuzisaka pointi tatu ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Stars ambayo ipo chini ya kocha Kim Poulsen imeondoka na ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania ambapo watatumia saa sita angani kabla ya kutua nchini humo.

Mpaka sasa kwenye kundi J, Tanzania inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne, Jamhuri ya Congo ikishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 5 mara baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Madagasca wakati Benin wakiwa vinara wa kundi hilo wakiwa na pointi saba.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!