May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maumivu watumiaji wa simu, miamala ya fedha

Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, amependekeza kuongeza gharama za kufanya mialama ya simu pamoja na gharama za laini. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Dk. Mwigulu, amebainisha hayo leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021, wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma.

“Kutoza kiasi cha Sh.10 hadi Sh.200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa watumiaji,” amesema

Amesema, pendekezo hilo litapelekea kuongeza mapato ya Serikali kiasi cha Sh.396.3 bilioni

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Pia, Dk. Mwigulu amesema, “kutoza tozo ya Sh.10 hadi Sh.10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au kutolewa.”

Amesema, pendekezo hilo litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha Sh. 1.2 trilioni

error: Content is protected !!