WAKATI wananchi wakiendelea kuugulia juu ya tozo za miamala ya simu, majengo na mafuta, Serikali inakuja na maumivu mengine ya tozo 17 za kazi mbalimbali za wasanii. Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea).
Baadhi ya maeneo yanayopendekezwa ni kwenye; vituo vya redio, televisheni, vituo vya kuuza mafuta vyenye vifaa vya muziki, maduka ya madawa ya binadamu, benki na taasisi nyingine za kifedha pamoja na maeneo ya kufanyia mazoezi ‘gym.’
Pia, maeneo yanayopiga karaoke, maonyesho kwa umma kwenye vyumba vya hoteli, viwanja vya ndege za ndani na za kimataifa, vyombo vya usafiri, maonyesho kwa umma katika mabaa, pubs, klabu na grosari na maonyesho kwa umma kwa kazi za filamu.
Maandalizi ya tozo hizo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyeagiza wizara ya habari, utamaduni, saana na michezo kuhakikisha ifikapo Desemba 2021, wasanii wanaanza kulipwa mirabaha.
Rais Samia alitoa maagizo hayo tarehe 15 Juni 2021, wakati akizungumza na vijana jijini Mwanza akisema “kuanzia Desemba 2021, wasanii wataanza kulipwa mirabaha kwa kazi zao zinazotumiwa katika radio, televisheni au mitandaoni.”
Tayari Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imeandaa kanuni ya leseni na haki ya kuuzwa tena kwa kazi za ubunifu zikiwa na viwango vya mapendekezo ya ada pamoja na sababu za kuanzishwa kwa tozo hizo.
Endapo mapendekezo hayo yatapitishwa na kuanza kutumika, utakuwa mzigo mwingine kwa wananchi ambao haohao wanaendelea kukamuliwa kwenye tozo za miamala ya simu, mafuta na majengo.
Undani wa habari hii na viwango vinavyopendekezwa kwa kina eneo, soma gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumamosi tarehe 21 Agosti 2021.
Leave a comment