Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS
Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love

ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil United Front – Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kati ya mwaka 2015 na Oktoba 2020, Maulid Mtulia, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya (DAS). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mtulia aliyeondoka CUF katika kile kinachoitwa, “kuunga mkono juhudi,” amepelekwa wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, kufanya kazi hiyo.

Katika orodha iliyotolewa na Ikulu ya Rais Samia Suluhu Hassan, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, tarehe 7 Juni 2023, jina la Maulidi Abdallah Mtulia, liko namba thelathini (30) kwenye orodha ya wateuliwa.

Maulidi Said Abdallah Mtulia, alitangaza kujiondoa CUF na kujiunga na CCM, tarehe 2 Desemba 2017. Alitangazwa tena kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, tarehe 18 Feb 2018.

Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe wakati anajiuzulu wadhifa huo, Mtulia alisema, atika barua yake ya kujiuzulu, Mtulia amesema amechukua maamuzi hayo, kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.

Alisema, ameamua kujiuzulu nafasi yake hiyo ya ubunge na kuhama chama, kuwa kumetokana na uzoefu aliyoupata kwa miaka miwili ya ubunge.

Aliongeza, “nimebaini kuwa serikali ya CCM, ambacho ni chama tawala, inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!