Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mauaji ya watoto Njombe yasisimua Bunge, serikali kujieleza
Habari za Siasa

Mauaji ya watoto Njombe yasisimua Bunge, serikali kujieleza

Joram Hongoli, Mbunge wa Lupembe (CCM)
Spread the love

BUNGE limeitaka serikali kuandaa na kutoa taarifa kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Njombe tangu kuanza kwa mwaka huu 2019. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ameitaka serikali kuandaa taarifa hiyo baada ya Joram Hongoli, Mbunge wa Lupembe (CCM) kuomba mwongozo wa Spika kama inawezekana kusitisha shughuli za Bunge hata kwa dakika 20 ili kujadili mauaji hayo.

“Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Njombe kuanza mwanzoni mwa mwaka huu Januari, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe watoto watatu walishauawa na baada ya hapo wameshahamia Halmashauri yangu ya Njombe kwa maana ya Jimbo la Lupembe.

“Mpaka ninavyoongea hivi watoto wanne tayari wameshauawa, watoto watatu kutoka kwenye familia moja na mtoto mmoja katika Kijiji cha Matembwe aliuawa siku ya Ijumaa na kuzikwa Jumamosi,” qmesema Hongoli na kuomba Bunge kuangalia uwezekano wa kujadili suala hilo kwa kina.

Spika Ndugai amesema, hoja iliyotolewa imeungwa mkono kwa kiwango ambacho hajawahi kuona “lakini kabla sijaamua, nimpe dakika mbili mbunge mmojawapo wa Njombe, nimekuona Mheshimiwa Deo Sanga na leo umepiga suti. Hebu tupe kidogo nini kinaendelea huko.”

Sanga amelieleza Bunge kuwa, hali ya Njombe ni tete kwa sasa kutokana na mauaji hayo na wageni wanaoingia kwenye mji huo hudhaniwa wamekwenda kuteka watoto.

“Na hivi sasa tunavyozungumza, baadhi ya biashara wakubwa wamekamatwa katika Mji wa Makambako katika Wilaya ya Njombe.

“Hao wafanyabiashara wakubwa wana siku nne ndani na hivi sasa, hatujui nini kinachoendelea, japo wafanyabiashara wengine walikuwa ni wakazi wa Makambako na walikuwa wako Dar es Salaam na ni wawekezaji wakubwa katika Mji wa Makambako hivi sasa wamekamatwa,” amesema na kuongeza;

“Na watu waliokamatwa mpaka sasa ni takribani watu 10 ambao ni wafanyabiashara wakubwa, kuna baadhi yao wana viwanda, wana watumishi zaidi ya 200. Shughuli sasa zimesimama na baadhi ya watu wengine wamewekeza hapo Njombe pia wafanyabiashara hao wakubwa.”

Jenista Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu amesema, jambo hili ni zito na linachukua taswira nzito ndani ya taifa.

“Tunadhani kwamba, sisi kama serikali ili tuweze kutoa maelezo ya kina, ni bora kiti chako kitupe nafasi tutayarishe kauli ya serikali na ili tuweze kuileta ndani ya Bunge lako haraka, Bunge lako liweze kujua hatua kubwa ambayo serikali tumechukua pia katika jambo hili,” amesema Jenister.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!