January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji ya vikongwe yaibuka Mwanza

Spread the love

WAKATI Taifa likitarajiwa kuingia katika uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais, watu wasiyofahamika wanadaiwa kuuwa kikongwe mmoja, Leticia Mwenda kwa kumkata mapanga, kichwani na shingoni. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo katika kata ya kishiri B wilaya ya Nyamagana, Mwanza ambako kikongwe huyo aliuawa saa 1.30 usiku.

Imeelezwa kuwa kikongwe huyo siku ya tukio alikuwa nje ya nyumba yake akipika wali kwa kutumia jiko la kuni na ndipo wauaji hao walifika na kuanza kumshambulia kwa kumkata shingoni, kichwani na kufariki papo hapo.

Inadaiwa kuwa wakati wauaji hao wakifanya hilo la kusikitisha, mtoto mmoja wa kikongwe huyo, Suzan Masanja alikuwa sokoni akiuza mchele na kwamba aliporejea nyumbani alimkuta mama yake akiwa ameuawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi, Charles Mkumbo, akizungumza na Mwanahalisi Online leo, alikiri kutokea tukio hilo na kuahidi polisi kushughulikia tukio hilo na kuwakamata watu waliyohusika.

Mkumbo amesema mpaka sasa wanamshikilia kijana mmoja, Maduhu Masanja ambaye alikuwa ni mkwe wa marehemu ambaye alikuwa ameachana naye kwa ajili ya uchunguzi wa tukio.

Kamanda Mkumbo amesema kwa mujibu wa upelelezi wa awali waliyoufanya inadaiwa kuwa kijana huyo aliwahi kuwatolewa vitisho wanafamilia wa marehemu huyo.

“Mtoto wa marehemu ametueleza mume wake baada ya kuachana naye, alitoa vitisho na baada ya vitisho walitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa na panga ambalo lilitumika kwenye mauaji tumelipata karibu na nyumba ya marehemu,” amesema Mkumbo.

Hata hivyo kamanda alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa polisi ili sheria zichukue mkondo wake.

Hilo ni tukio la nne katika eneo hilo la Kishiri watu kuuawa kwa kukatwa mapanga akiwamo askari aliyeuawa hivi karibuni akiwadaiwa kuiba mafuta eneo la mnara wa mitandao ya simu na kusababisha wenyeviti wawili wa mtaa wa Kishiri B na Kanindo kushikiliwa na polisi hadi sasa.

error: Content is protected !!