Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mauaji ya Jamal Khashoggi, CIA yaivua nguo Saudia Arabia
Kimataifa

Mauaji ya Jamal Khashoggi, CIA yaivua nguo Saudia Arabia

Mwandishi Jamal Khashoggi enzi za uhai wake
Spread the love

 

RIPOTI mpya iliyotolewa na shirika la kijasusi la Marekani (CIA), imemtaja mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia Arabia, Mohammed Bin Salman, ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya mwandishi habari, Jamal Khashoggi (59). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Khashoggi alifariki duni mwaka 2018, katika ubalozi wa Saudia, mjini Intanbul, nchini Uturuki,

Ripoti hiyo ya shirika la kijasusi iliyotolewa na utawala wa Rais Joe Biden, imeeleza kuwa Bin Salman aliidhinisha operesheni ya kumkamata; na au kumuua Khashoggi, mjini Istanbul, nchini Uturuki.

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani, Antony Blinken amesema, kufuatia kupatikana kwa taarifa hiyo, serikali ya mjini Washington, itachukua mwelekeo mpya wa kisera kwa taifa hilo la Saudia.

Hata hivyo, serikali mjini Riyadh na mwanamfalme mwenyewe, wamekana kuhusika na mauaji hayo na kusema, taarifa hiyo imejaa uzushi na inatathmini isiyokubalika kuhusu utawala wa falme.

Serikali ya Saudia imekuwa ikieleza kuwa mauaji ya Khashoggi kwenye ubalozi wake mdogo, nchini Uturuki, yalifanywa katika operesheni ya kihalifu na inakanusha mwanamfalme Salman kuhusika na mauaji hayo.

Aidha, Saudi Arabia inapinga kile inachokiita, “kuingiliwa kwa utawala wake na uhuru wa mfumo wake wa mahakama.”

“Ripoti hii, imekuwa na hitimisho lisilo sahihi. Imetolewa wakati falme hii imekwisha kosoa uhalifu huo wa kutisha, na uongozi wa Saudia umechukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena,” imeeleza taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni ya taifa hilo.

Mrithi huyo wa kiti cha ufalme –  Mohammed Bin Salman – ameendelea  kukanusha madai hayo, pamoja na washauri wake kadhaa wa karibu, kutiwa hatiani kwa mauaji hayo na mamlaka za sheria nchini humo.

Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani akiandika ripoti zinazomkosoa Mohammed Salman na serikali ya Saudia, aliuwawa tarehe 2 Oktoba 2018.

Mwandishi huyo alielezwa na balozi wa Saudia afike katika ubalozi wa taifa hilo mjini Istanbul, ili aweze kupatiwa nyaraka kadhaa alizokuwa akizihitaji kumuwezesha kufunga ndoa na mpenzi wake Hatice Cengiz, raia wa Uturuki.

Wakati Saudia ikikana kuhusika na mauaji hayo, ripoti ya kijasusi imesheheni ushahidi unaonyesha ushirka wa Bin Salman katika mauaji hayo.

Saudi Arabia, ni mshirika muhimu wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

CIA inaeleza kwa kujiamini, kwamba Bin Salman, ndiye aliyeamuru mauaji hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Xi Jinping awasili Urusi, kufanya mazungumzo na Putin

Spread the love  RAIS wa uchini Xi Jinping amewasili sasa nchini Urusi,...

Kimataifa

Maandamano Kenya, Afrika Kusini yashika kasi, wapinzani wakishikiliwa

Spread the love  MAANDAMANO ya kupinga serikali zilizoko madarakani nchini Kenya na...

Kimataifa

Maandamano Afrika Kusini: Tanzania yatahadharisha raia wake

Spread the love  WAKATI maandamano yaliyoitishwa na Chama cha upinzani Afrika Kusini,...

Kimataifa

ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa rais Vladmir Putin wa Urusi

Spread the love  MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC) imetoa...

error: Content is protected !!