October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji ya Floyd: Hali ilivyo miji 25 Marekani

Spread the love

MAUAJI yaliyofanywa na polisi wa Mji wa Minnesota, yamebadili taswira ya miji 25 ya Marekani na kuwa ya vurugu, maandamano na uharibifu wa mali. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Licha ya kuwepo kwa wito kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu ikiwemo mameya, magavana wa majimbo, wananchi wa taifa hilo wanaamini unyama wa polisi kwa raia weusi umezoeleka, hivyo wameendelea kuonesha hasira zao dhidi ya upuuzi huo.

Idadi ya majimbo ambayo watu wanaingia mtaani kupinga unyama wa polisi weupe wa taifa hilo, inaongezeka kila kukicha.

San Francisco

London Breed, Meya wa San Francisco asubuhi ya leo tarehe 31 Mei 2020, ameeleza wasiwasi wake kutokana na idadi kubwa ya waandamanaji wakiwa na hasira dhidi ya serikali hasa kutokana na mauaji ya watu weusi.

Hata hivyo amesema, jimbo lake linaweka mkakati sawa kuhakikisha, kuanzia Jumapili ya leo, mazingira ya amani yanaimarishwa.

“Watu wameumizwa sana, wana hasira nami nina hasira pia,” Breed ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter na kuongeza “polisi watahakikisha kunakuwa na maandamano ya amani, kama tufanyavyo siku zote. Hatuwezi kuvumilia vurugu zinazoendelea kwa sasa.”

Marehemu George Floyd enzi za uhai wake

Biden: Mauamivu yetu yasituvuruge

Joe Biden, mteule wa Chama cha Democratic kuelekea uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu amesema, licha ya kuwa makosa yamefanyika, lakini maumivu waliyokuwa nayo wananchi yasivuruge taifa hilo.

“Sisi ni taifa, tunapaswa kutoruhusu mauamivu haya kutuvuruga. Kila mmoja wetu anaweza kueleza ubaya wa matabaka ya rangi hapa kwetu kama inavyoelezwa katika mauaji mabaya ya George Floyd.

“Kufanya maandamano kutokana na mauaji ya namna hii ni haki na wajubu lakini kuvunja na kuchoma moto vitu sio haki. Vurugu zinazohatarisha hazikubaliki. Vurugu zinazopelekea biashara kufungwa, hizo hapana.”

 Eric Garcetti, Meya wa Los Angeles

Eric Garcetti, Meya wa Los Angeles amesema, walinzi wa kitaifa (National Guard) watajumuishwa na walinzi wa jimbo hilo kuhakikisha usalama unarejea.

Amesema, hali hiyo inatokana na tishio kubwa linalokuja hapo mbele kutokana na ukubwa na wingi wa watu jimbo hilo ambao wamejitokeza kwenye maandamano. Los Angeles ndio mji wa pili kwa ukubwa na watu wengi Marekani.

Ili kupata msaada huo, Jumamosi tarehe 30 ameeleza kuwasiliana na Gavana wa California, Gavin Newsom ili kupata nguvu ya kuyakabili maandamano hayo.

Amemwomba Newsom kumsaidia polisi 500 – 700. Waandamanaji kwenye mji huo wameharibu magari ya polisi, wameharibu na kubomoa maduka pia kupambana na polisi uso kwa uso.

Mji wa Salt Lake

Waandamanaji wameendelea kujitokeza kwenye Mji wa Salt Lake, hata hivyo polisi wa mji huo wameeleza kujiandaa kuwapa muda wa kuondoka maeneo ambayo watu wamekusanyika sambamba na kukamata watakaokaidi.

Maandamano makubwa yalianza kushuhudiwa jana Jumamosi na kwamba, mpaka sasa polisi wameeleza kukamata watu sita wakihusisha na kuendesha maandamano hayo. Magari na vitu mbalimbali tayari vimeharibiwa

Washington, DC

Mamia wa waandamanaji wameelekea viwanja vya Ikulu ya Marekani kupinga unjama ulioendeshwa na polisi na kusababisha kifo cha Floyd.

Kwenye maandamano hayo, walibeba mabango yaliyoandikwa maneno ya mwisho ya Floyd ‘siwezi kupumua,’ huku mengine yakiandikwa ‘hakuna haki.’ Jijini humo maandamano yanaripotiwa kuwa ya amani.

Hata hivyo, magari ya maji ya washa na polisi waliovalia ‘kikazi’ walikuwa kwenye lango la Ikulu hakuhikisha hakuna mtu anayefika eneo hilo

Watu 1,400 wakamatwa

Kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo, polisi wameeleza kukamata watu 1,400 katika majimbo 25 yanayotajwa kukithiri kwa vurugu kutokana na mauaji ya Floyd.

 

Jiji la New York

Polisi jijini humo wanaendelea kumsaka muandamanai mmoja aliyerusha mawe kwenye majari lao na kusababisha uharibifu. Polisi ha waliendesha gari kuelekea kwenye eneo la vizuizi na ndipo walipoanza kushambuliwa.

Magari hayo yalielekezwa kwenye kundi la watu na kusababisha mtafaruku huku watu kadhaa wakigonjwa.

Meya wa Nashville aomba msaada

John Cooper, Mayor wa Nashville ameingia mashaka kutokana na waandamanaji kuunguza baadhi ya maeneo huku akitangaza kuwepo kwa hali ya hatari.

Waandamanaji walivamia eneo la mahakama ya mji huo na kuchoma moto wakipinga unyama na ubaguzi wa rangi unaoendeshwa na polisi wa Marekani.

Maelefu ya watu katika mji huo, wameendelea na maandamano wakitaka polisi waliofanya unyama huo wachukuliwe hatua na kukomesha vitendo hivyo. Kutokana na maandamano hayo, maeneo mbalimba ya serikali yameharibiwa.

Trump amng’ang’ania Meya Minneapolis

Wakati maandamano yakiendelea kwa siku ya tano sasa, Donald Trump, rais wa taifa hilo ameendelea kumwangushia lawama Meya wa Minneapolis kwamba ameshindwa kazi ya kutuliza vurugu.

“Polisi wa Kitaifa wametumwa kwenda kutuliza amani katika mji wa Minneapolis, kazi ambayo Meya wa Mji huo anayetokana na chama cha Democratic ameshindwa,” amesema.

Chicago

Waandamanji wameendelea kuonesha hasira zao hasa wakikumbuka mauaji ya namna hiyo yaliyofanywa mwaka 2014.

Ni kipindi ambacho polisi walifanya mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 17, Laquan McDonald na kusababisha taharuki. Tukio la Lyody linawafanya wakazi wa mji huo kuamini kwamba, unyama wa polisi wa Marekani upo kwenye damu yao.

Texas

Idadi kubwa ya waaandamanaji wenye hasira imemsukuma Gavana wa Texas, Greg Abbott kupeleka zaidi polisi 1,500 kwenye maeneo ya watu walipokusanyika.

Hata hivyo amesema, polisi wengine watakwenda kukabiliana na waandamanaji katika maeneo ya Houston, Dallas, Austin na San Antonio na kwamba kumekuwa na upinzani mkali mkubwa kutoka kwa waandamanaji.

Mkuu wa Polisi Houston, Art Acevedo ameeleza kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba, mpaka Jumamosi watu zaidi ya 200 kwenye eneo lake tayari wamekamatwa.

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika kwenye kituo cha polisi cha Austin wakishinikiza unyama aliofanyiwa Floyd ukomeshwe.

Chicago

Kwa siku ya pili mfululizo, waandamanaji wamekufanyika mbele ya kituo cha polisi cha Chicago. Polisi licha ya kuwataka watu hao waondoke, hawakuondoka. Inaripotiwa waandamanaji zaidi ya 100 wamekamatwa.

error: Content is protected !!