Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mauaji wivu wa mapenzi yatikisa 2020
Habari Mchanganyiko

Mauaji wivu wa mapenzi yatikisa 2020

CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi
Spread the love

MATUKIO ya mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi, yameongoza katika mwaka 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar Es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 21 Desemba 2020 na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Liberatus Sabas wakati akieleza hali ya usalama nchini.

Bila kutaja idadi ya vifo hivyo, Kamanda Sabas amesema, chanzo chake ni mmomonyoko wa maadili, na kuwaomba viongozi wadini na Watanzania kwa ujumla waingilie kati kupunguza vifo hivyo.

“Haya ni mauaji ambayo yana hitaji sana kutoa elimu lakini pia kushirikisha wadau wengine wakiwemo viongozi wa dini. Mfano matukio ya mauaji kutokana na wivu wa mapenzi ambaypo kwa sas ndio yanaongoza.

Viongozi wa dini tuna amini watatoa mchango mkubwa sana, sababu yanatokana na mmomonyoko wa maadili,”amesemaKamanda Sabas.

Licha ya matukio yanayotokana na wivu wa mapenzi, Kamanda Sabas amesema vifo vingine vimetokana na imani za kishirikina na baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

“Matukio mengi ya mauji yana tokana na  imani za kishirikiana, vifo vya mapenzi lakini pia wananchi kujichukulia sheria mkononi,” amesema Kamanda Sabas.

Aidha, Kamanda Sabas amesema matukio ya mauaji kwa kutumia silaha katika mwaka 2020 yalidhibitiwa.

“Matukio ya mauaji kwa kutumia silaha yamedhibitiwa kwa kiwango kikubwa, pia hata matukio ya mauaji kutokana na uhalifu mwingine yamepungua kwa kiasi kikubwa,” amesema Kamanda Sabas.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!