July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji tena Mwanza

ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Spread the love

JIJI la Mwanza linakithiri kwa mauaji ambapo leo watu wawili wamemfyatulia risasi kifuani na begani, Aliphonce Musanyenzi, Mwenyekiti wa Serikali Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa na kumuua, anaandika Moses Mseti.

Tukio hilo linakuja ikiwi ni siku nne tangu watu watatu waumini wa Dini ya Kiislamu kuuawa msikitini jijini humo.

Katika kipindi cha mwezi mmoja sasa watu zaidi ya 11 wamepoteza maisha kutokana na kuendelea kuwepo kwa matukio ya kinyama yanayofanywa na vikundi vya watu visiofahamika.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamikia leo saa 2: 00 usiku wakati Musanyenzi akiwa katika harakati za kusuluhisha ugomvi wa familia ya Neema Malangula na anayetajwa kuwa bwana wa Neema ambaye hajafamika.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, wakati mwenyekiti huyo akiwa na familia hiyo, ghafla walitokea watu wawili watembea kwa mguu na kuwaambia kwamba wapo chini ya ulinzi.

Baada ya kuwaamru, ndipo watu hao waliokuwa wawili, mmoja wao alimfyatulia risasi za kifuani na begani Musanyenzi na kufariki dunia.

Diru Luzerera, Shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo amesema kuwa, alitoka na marehemu katika kikao cha ulinzi na usalama wa mtaa huo saa 12 jioni.

Luzerera amesema kuwa,” marehemu Musanyenzi baadaye tukiwa kwake alituambia twende duka lililopo kwake akatununulie soda, tulipomaliza kunywa soda na wakati anatusindikiza ndipo tulikumbana na watu hao,” amesema.

Getruda Henry, mke wa marehemu Mumusanyenzi amesema kuwa, katika familia yao hawakuwa na ugomvi na mtu yeyote.

“Nikiwa shambani naendelea na shughuli zangu, ndipo nikasikia kelele watu wakikimbia hovyo na mimi nikakimbia kuelekea nyumbani ile nafika tu, nikakutana na watu wakiwa wamezunguka nyumba huku mume wangu (Alphonce Musanyenzi) akitokwa damu,” amesema Henry.

error: Content is protected !!