May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji Atlanta: Joto la chuki lapanda

Spread the love

 

KATI ya raia wanane walioshambuliwa na kupoteza maisha Atlanta, Georgia nchini Marekani, sita ni Wamarekani wenye asili ya Asia. Inaripoti mitandao ya nje … (endelea).

Kutokana na mauaji hayo yaliyotokea jana Jumatano, tarehe 16 Machi 2021, Korea Kusini imefikisha malalamiko yake kwa Joe Biden, Rais wa Marekani kulaani kulengwa kwa wananchi wenye asili ya Asia.

Taarifa zinaeleza, raia wa Wamarekani wenye asili ya Asia wamekuwa wakilengwa katika miezi ya karibuni wakihusishwa na kusambaza virusi vya corona (COVID-19).

Raia hao wameeleza kuishi kwa hofu kutokana na kushambuliwa mara kwa mara sambamba baadhi yao kutengwa na kuonekana hawafai.

Sita kati ya wanane waliouawa kwenye shambulio hilo wanatoka Korea. Rais Bideni ameita shambulio hilo kuwa ‘la kinyama.’

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 21, anashikiliwa na polisi kwa madai ya kuhusika kwenye shambulio hilo. Hata hivyo, bado haijaelezwa lengo la shambulio hilo.

Mauaji hayo yametokea kwenye maeneo mawili tofauti, maeneo hayo ni Gold Massage Spa na Aroma Therapy spa.

error: Content is protected !!