August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matusi ya CCM yatikisa Bunge

Spread the love

KAULI ya ‘matusi’ iliyotolewa jana na Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), imesababisha wabunge wanawake kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutimuliwa nje, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Jana Mlinga alitoa kauli iliyotafsiriwa na wabunge hao kwamba, ndani ya Ukawa ili wabunge hao wapate nafasi hizo lazima ‘wachojoe.’

“Mheshimiwa Spika, kuthibitisha hilo ili upate ubunge ndani ya Kambi ya Upinzani lazima uitwe ‘baby’.

“Watu hawa wamefikia hatua ya kuwa na mahusiano ya jinsia moja,” alisema Mlinga. Kauli hiyo imesababisha mtifuano leo na kupelekea Job Ndugai, Spika wa Bunge kuwatoa nje wabunge hao.

Wabunge hao wanawake walianza kufanya fujo ndani ya Ukumbi wa Bunge baada ya Mlinga kushindwa kuomba radhi kutokana na madai ya kuporomosha matusi dhidi ya wabunge hao.

Kabla ya kutolewa nje, wabunge hao waliomba muongozo kutoka kwa spika kutaka Mlinga afute kauli yake, spika hakuruhusu na hapo ndipo fujo zilianza kuibuka.

Wabunge ha wametafsiri kitendo hicho kama udhalilishaji ambapo wamepanga kuiandikia barua Ofisi ya Bunge ikiwa ni pamoja na kutishia kujitoa katika Chama cha Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Tanzania.

Wameeleza kuwa, kukaa kimya kwa wabunge wanawake wa CCM kunaonesha kuridhika na matusi waliyoporomoshewa hatua ambayo wameeleza kutoifumbia macho.

error: Content is protected !!