Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Matumizi ya mbegu bora yaongezeka kwa kasi
Habari Mchanganyiko

Matumizi ya mbegu bora yaongezeka kwa kasi

Spread the love

MATUMIZI ya mbegu bora za mazao mbalimbali hapa nchini yameongezeka kwa sasa kutoka asilimia 20 iliyokuwa miaka ya nyuma  hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2018 kufuatia wakulima kuanza kuielewa elimu ya matumizi ya mbegu bora na kuleta tija ya kilimo hapa nchini. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Hayo yalisema leo na Mkaguzi mwandamizi wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Emmanuel Mwakatobe kwenye mdahalo wa haki ya mbegu kwa wakulima wadogo ambao umeandaliwa PELUM Tanzania, na kusema karibu asilimia kubwa ya wakulima wote waliopo Tanzania wamekuwa wakitumia mbegu zisizo rasmi kufuatia kukosa elimu ya mbegu bora.

Amesema kuwa matumizi ya mbegu zisizo rasmi yameendelea kusababisha wakulima kukosa mavuno kidogo na kutokidhi haja ya mahitaji ya kifamilia na hata kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla.

Mwakatobe amesema kuwa matumizi ya mbegu bora yanaongezeka zaidi ukilinganisha na kipindi kilichopita kufuatia kuona tija ya mbegu bora kwa sasa kwani zamani wakulima walikuwa wakitumia mbegu za kwa jirani au shambani ambazo hazijakidhi ubora kutokana na kutokuwa na uelewa.

“Kuna aina tatu za mifumo ya mbegu ambayo ni mfumo rasmi, usio rasmi na mchanganyiko, kwa sasa tunapaswa kutumia mfumo ulio rasmi kwa kuongeza tija kwenye kilimo,” amesema.

Hivyo amewashauri wakulima kuona umuhimu wa kutumia mbegu bora sababu zinazaa zaidi ambapo alitolea mfano mbegu ya mpunga ijulikanayo kama TXG 306 ambayo inauwezo wa kutoa mazao zaidi ya gunia 38 kwenye hekari moja ambayo ni tofauti ya mbegu zisizo rasmi ambazo mkulima huweza kupata gunia 5 kwa hekari moja.

Naye Mkulima na mzalishaji wa mbegu za kuadhimiwa ubora (QDS) kutoka Dodoma, Mathias Mtwale alikiri kuwepo kwa matumizi ya mbegu zisizo rasmi kwa wakulima na kusema kuwa hali hiyo inatokana na uchache wa biashara ya mbegu  na kukosena kwa makampuni ya kuweza kuwafikia wakulima.

Amesema kuwa uzalishaji wa mbegu bado ni changamoto kubwa kwa wakulima wa ndani kwani zaidi ya kutumia mbegu zisizo rasmi wamekuwa wakikumbana na mbegu kutoka nje ya nchi ikiwemo Kenya.

Mkurugenzi wa Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya shughuli za kuendeleza na kuhamasiha kilimo cha kiikolojia nchini Tanzania (PELUM- Tanzania), Donati Senzia ambaye ni amewashauri wakulima kutumia mbegu zilizo rasmi ili kuweza kuongeza tija kwenye kilimo.

Senzia amesema kuwa lengo la mdahalo huo ni kuamsha uelewa kwa wakulima juu ya mifumo ya sera na sheria zinazosimamia taratibu za mbegu bora za mazao ya kilimo Tanzania.

Pia Senzia amesema, watajadiliana na kutoa mapendekezo namna gani bora ya mifumo ya mbegu inavyoweza kumsaidia na kumnufaisha mkulima mdogo kufuatia zaidi ya asilimia 90 ya chakula kinazalishwa na wakulima wadogo na zaidi ya asilimia 80 wanatumia mbegu zinazotoka katika mfumo usio rasmi.

Hivyo amesema kuwa majadiliano hayo yataboresha namna ya mifumo ya usimamizi na udhibiti wa mbegu kisera na kisheria kwa lengo la kuongeza tija na kipato na kuondoa umaskini kwa wakulima Tanzania.

Senzia amesema Mdahalo huo pia umelenga kuwasaidia wakulima kufuatia shughuli za PELUM kwa sasa kuwa zinahusisha haki za ardhi za wakulima wadogo, ufikiaji wa masoko, bajeti inayomnufaisha mkulima mdogo pamoja na haki za mbegu kwa mkulima mdogo ambapo mdahalo huo umehusisha wadau mbalimbali wa mbegu wakiwemo kutoka mkoani na wizarani na watafiti mbalimbali ili kujadiliana na kutoa mapendekezo ya kumnufaisha mkulima mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!