January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matumizi ya BVR kura ya maoni kushidwa

Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Msatafu Damian Lubuva kuwa Mkwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),

Spread the love

MRADI wa vitambulisho vipya vya kupigia kura, vitakavyotumika kupitishia Katiba Pendekezwa, umekwama. Anaripoti Pendo Omary…… (endelea).

Vitambulisho hivyo vipya vinavyoandaliwa kupitia teknolojia mpya ya “Biometric Voters Registration (BVR), havijafunguliwa na kuunganishwa; jambo ambalo linatia shaka ufanikishaji wa mradi mzima.

“Baadhi ya vifaa vilivyopokelewa na NEC (Tume ya Taifa ya uchaguzi) kama vile vitunza kumbukumbu (servers) vinakilishi, mashine za kuchapa na vinginevyo, bado vimefungiwa ofisini na wala haijulikani, ni lini vitajaribiwa,” anaeleza mtaalam mmoja wa vifaa hivyo ndani ya NEC.

Mfumo wa BVR unatumika kuchukua taarifa za mtu kibaiolojia au tabia za mwanadamu na kuzihifadhi katika kazidata (database) kwa ajili ya utambuzi.

Anasema, ikiwa zimebaki siku 39 kabla ya kufanyika kura ya maoni kuhusu Katiba Pendekezwa, NEC haijaanda mtandao wa akiba wa kuwezesha taarifa zilizotunzwa zisipotee (disaster recovery site), pale inapotokea mtandao wa kuhifadhi taarifa umehujumiwa au umeshindwa kufanya kazi kutokana na matatizo mbalimbali.

Taarifa zinasema, mpaka sasa – siku 39 kabla ya kufanyika kura ya maoni – vifaa vilivyopo ni 250 ambayo vilitumika katika majaribio ya mradi katika jimbo la Kawe, Kilombero na Mlele, Desemba mwaka jana.

“NEC ilisema inahitaji vifaa 15,000; lakini serikali imesema ina uwezo wa kutoa vifaa 8,000. Mpaka sasa, zikiwa zimebaki siku 39, NEC imekabidhiwa vifaa 250 tu. Hakuna dalili ya vifaa vingine kuletwa. Kwa ufupi, zoezi hili limeshidwa,” ameeleza mtia taarifa wetu.

Mtoa taarifa anasema, licha ya NEC kuwatangazia wananchi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura katika halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe, kuanzia tarehe 23 Februari hadi 1 Machi, zoezi hilo halitafanikiwa.

Mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh. 293 bilioni.

Mtaalam wa mfumo huo ameweka angalizo kuwa NEC isijaribu kutumia njia ya utumaji taarifa bila ya kuingia mkataba maalumu wa usafirishaji taarifa hizo unaoitwa Service Level Agreements na mashirika ya simu.

Anasema, hatari ya kuingia katika matumizi hayo bila kuwapo mkataba, kwa kuwa mfumo huo unaruhusu muingiliano wa taarifa kati ya watumiaji wa kawaida na taarifa za NEC.

error: Content is protected !!