Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Matukio uvunjifu wa haki kukusanywa kidigitali
Habari Mchanganyiko

Matukio uvunjifu wa haki kukusanywa kidigitali

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimezindua mfumo wa kidigitali wa kukusanya taarifa za matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizindua mfumo huo leo tarehe 3 Mei 2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga amesema, wamefungua mfumo huo ili kuondoa changamoto ya utoaji wa taarifa kwa Watanzania.

Wakili Henga amesema mfumo huo utasaidia kuondoa changamoto ya utoaji wa taarifa za matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa kuwa ni rahisi na hauchukui muda mrefu, pamoja na kulinda usalama wa watoa taarifa.

 “LHRC tunautambulisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa na matukio ya uvunjifu wa haki za kibinadamu kwa njia za mtandao, kama mtu ameumizwa amenyang’anywa shamba lake, badala ya kutupigia simu   za mkononi au anakuja kituoni anautumia mfumo huo,” amesema Wakili Henga.

Amesema kabla ya mfumo huo kuzinduliwa, wananchi walikuwa wanashindwa kutoa taarifa na kupata msaada wa kisheria kutokana na kutokuwepo kwa njia rafiki za utoaji wa taarifa, pamoja na uchache wa watoa msaada wa kisheria.

“Kituo kilifikiria njia hii baada ya kuona kuna changamoto kubwa ya utoaji taarifa hasa kwa wananchi na walinzi wa haki za binadamu walioko nje hasa kijijini, mfumo huu tutakuwa kila mahali na watu kupata fursa ya kutoa taarifa,”

 “Njia ya kutumia Wasaidizi wa kisheria ilikuwa inachukua muda mrefu , tumezindua mfumo huu ili kurahisisha zaidi, kukusanya taarifa za matukio zake na utatumika kwa wananchi wote wa Tanzania,” amesema Wakili Henga.

Mfumo huo hupokea taarifa kwa njia tatu ikwiemo njia ya mtandao kwa kutafuta https://hrms.humanrights.or.tz, njia ya pili ni kwa njia ya simu janja aina ya Android ambapo kuna program ‘App’ ya LHRC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!