May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matola awaita mashabiki Uwanjani

Seleman Matola kocha msaidizi wa klabu ya Simba

Spread the love

KOCHA msaidizi wa Simba Suleiman Matola, awataka washabiki wa simba wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi klabu ya Yanga, kwasababu timu yake imejiandaa vyema. Anaripoti Jemima Samwel DMC (endelea)

Mchezo huo utapigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni.

Kocha huyo msaidizi ametoa kauli hiyo hii leo Tarehe 7 Mei 2021 katika mkutano wa waandishi wa habari  na kusema kuwa kikosi chake kimejipanga vyema na mchezo wa kesho na kuwahahakikishia ushindi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

“Maandaliz yetu sisi  yanaendelea vinzuri na hakuna mchezaji yeyote tunaweza kumkosa  kesho na hatuna majeruhi wala hakuna mchezaji aliyopewa adhabu yeyote ni jambo la kumshukuru Mungu pia.”Matola amesema.

“Washabiki wajitokeze kwa wingi kuja kuangalia mechi maana tumejipanga haswa katika mechi hii na wachezaji wapo kambini  kwa ajili ya hii mechi kwahiyo kujitokeza kwa wingi ni muhimu.” Alisema Matola

Timu hizo zinakutana mara ya pili kwenye msimu huu ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga alikuwa mwenyeji ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mpaka sasa timu hizo zipo juu kwenye msimamo wa Ligi ambapo Simba ipo kileleni wakiwa na pointi 61 mara baada ya kucheza michezo 25, huku nafasi ya pili ikishikwa na Yanga wenye pointi 57 mara baada ya kucheza michezo 27.

error: Content is protected !!