June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matokeo kura za maoni Dodoma hadharani

Mbunge wa Jimbo la KIbakwe, George Simba Chawene

Spread the love

MATOKEO ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa wa Dodoma yametangazwa rasmi na kuwataja washindi katika majimbo hayo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM wilaya ya Chamwino ambaye ni Mkurugenzi wa uchaguzi katika kura za maoni katika wilaya ya Chamwino yenye majimbo mawili Janeth Mashele amesema matokeo hayo hayamfanyi mshindi katika kura za maoni kujiakikishia ushindi huo kwani bado kuna vikao vya uteuzi ndani ya CCM.

Akitangaza makoteo katika jimbo la Chillonwa,alimtaja Makanyaga Mwaka kuwa mshindi katika kura za maoni kwa kupata kura 6,999,ambapo mpinzani wake Deo Ndejembi ambaye alipata kura 5,500 na Mapana Elisha ambaye alipata kura 4278.

Katika jimbo la Mtera mbunge ambaye alikuwa akitetea nafasi yake Livingstone Lusinde aliibuka kidedea kwa kupata kura 20,724,akifuatiwa na Samuel Malecella ambaye alipata kura 3,835 na kufuatiwa na Ulaya Stevan alipata kura 2,731.

Wakati huo aliyekuwa katibu wa Chadema Wilaya ya Chamwimo Lameck Lobote ambaye alihamia CCM na kugombea ubunge ameshindwa kwa mbali kwa kupata kura 406.

Akitangaza majimbo mwingine Katibu wa CCM mkoa Albert Mgumba ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi CCM mkoa alimtaja mbunge wa Kongwa ambaye alikuwa akitetea nafasi yake Job Ndugai kwa kuibuka kidedea kwa kura 22,599, akifuatiwa na John Pallango kura 2,566 huku Dk. John Chilongani akiambulia kura 2,563.

Katika jimbo la kibakwe Mbunge anayetetea nafasi yake George Simba Chawene ameibuka kidedea kwa kupata kura 18,158 akifuatiwa na Mwanyinge Mwikola kura 6,901 huku Akley Galawika kura 5,562.

Kwa upande wa kondoa Mjini, Sanda Edwini kura, 2,626 ambapo aliyekuwa akitetea kiti chake Mahita Zabein kura 1,539 na Nyangani Ahammed kura 639.

Kwa upande wa Kondoa Vijini,Dk Ashatu Kijaji ameibuka kwa kura 9,162, Lubuva Hasani kura 9,113 na Monica Mohamed kura 4,641.

Jimbo la Chemba Juma Nkamia kura 17,406,Costantino Degera kura 1,777 na Khamis Mkotya kura 1,420.

Wakati huo huo majimbo mawili majimbo mawili ya Dodoma mjini na Bahi majibu yanasuasua kutangazwa.

Katika jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka ameibuka Kidedea kwa kupata kura 6972 huku mpinzani wake Dk.Pius Chaya akiwa na kura 6270.

error: Content is protected !!