Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Matokeo kidato cha nne, Shule za serikali hoi
ElimuTangulizi

Matokeo kidato cha nne, Shule za serikali hoi

Katibu Mkuu wa Necta, Dk. Charles Msonde
Spread the love

MATOKEO ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana (2016) yametolewa leo ambapo shule za serikali zimeendelea kufanya vibaya huku zile za binafsi zikipeta, anaandika mwandishi wetu.

Katika matokeo hayo jumla ya wanafunzi 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu ambapo madaraja yanayohesabika kama ufaulu ni kuanzia daraja la kwanza mpaka la nne.

Miongoni mwa shule kumi zilizoongoza hakuna shuke yoyote inayomilikiwa na serikali. Shule ya Feza Boys imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na St. Francis Girls, Kaizirege Junior na Marian Girls huku Marian Boys ikishika nafasi ya tano.

Matokeo hayo pia yanaonesha kuwa wavulana wamefaulu kwa asilimia 73.26 huku wasichana wakifaulu kwa asilimia 67.06.

Katika hatua nyingine, shule sita kati ya kumi za mwisho zimetoka katika Jiji la Dar es Salaaam.

Shule hizo ni pamoja na; Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Somangila, Mbondole na Kidete ambazo ni za serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Janeth Mbene apongeza HKMU, ataka wahitimu wajiajiri

Spread the loveWAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), ...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za SiasaTangulizi

⁩ Samia aridhia Chongolo kujiuluzu

Spread the loveMwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano ameridhia...

Habari MchanganyikoTangulizi

13 wafariki dunia ajali ya basi likigonga treni Singida

Spread the loveJUMLA ya watu 13 wakiwamo wanawake sita na wanaume saba...

error: Content is protected !!