May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matiko aibua hoja mpya miradi ya maji

Esther Matiko

Spread the love

 

MBUNGE asiye na chama, Esther Matiko amelishauri Bunge liunde kamati maalum kwa ajili ya kuchunguza miradi ya maji yenye harufu ya ubadhirifu. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Matiko ametoa ushauri huo leo Jumatatu tarehe 10 Mei 2021, akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2021/2022, bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo viti maalum ameshauri uchunguzi huo ujikite zaidi katika Mradi wa Usambazaji Maji katika miji 28 nchini, akisema kwamba kuna viashirifu vya ubadhirify wa fedha za umma.

“Nashauri ifanyike uchunguzi wa kina hata Bunge lako kupitia kamati yake ya maji,  iunde tume ipitie huu mradi tuhakikishe tunaenda na review ya mwanzo kuliko hii inayosema inapunguza idadi ya miji. Hata hiyo miji 24 wakibahatika kupata, mtandao wa maji utapungua,” amesema Matiko.

Matiko amesisitiza “haiwezekani miji hiyo kuounguzwa, kuna harufu ya uendelevu wa ubadhirifu wa fedha. waziri anajitahidi lakini bila kung’oa mizizi ya ubadhirifu wa fedha hili suala litaendelea.”

Mradi wa usambazaji maji katika miji 28, unaobeba zaido ya miradi 1,423 ulianza kuetekelezwa Disemba 2019, kwa gharama ya Sh. 1.3 Trilioni, fedha za mkopo kutoka Serikalo ya India.

Akiuelezea mradi huo, Matiko amesema mradi huo una dosari kufuatia hatua ya kupunguzwa idadi ya miji pamoja na mtandao wa maji.

“Miji 28 ambayo Tarime ilikuwemo ni dhahiri ingeweza kutusaidia sana lakini kuna fununu baadhi ya miji itaondelewa ikiwemo Tarime, Songea na Mafinga. Charles Kitwanga mwaka jana alisema hspa bungeni kwa uchungu, ule mradi wa dola 460 milioni  (Sh.Tril. 1.3) zingeweza kutosha miji 54, akaelezea kuna harufu wya upotevu wa fedha,” amesema Matiko.

Matiko amehoji “badala ya miji kuwa 28 wanapunguza iwe 24. Na mtandao wa maji wanaounguza kutoka kilomita 5,751 kwenda 5711,  unajiuliza kama wanapunguza tungetarajia gharama ingeenda chini ya hapo lakini halijafantika, fedha zingine zinaenda wapi?”

Mbali na madai ya kupunguzwa kiwango cha mtandao wa mradi huo, Matiko amesema visima 44,590 kati ya 131,370 vilivyochimbwa kupitia mradi huo, havitoi maji.

“Miradi iko 1,423 ambayo ilikuwa na visima  131,370  na visima hivyo 86,000 visima vinatoa maji na 44,590 havitoi maji, fedha hazifuatiliwi zinapotea wanashindwa kufikia malengo,” amesema Matiko.

Aidha, Matiko ameshauri watu watakaobainika kufanya ubadhirifu katika miradi ya maji, wachukuliwe hatua.

error: Content is protected !!