January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matenki 3,250 yakuvunia maji yajengwa

Tanki la kuvuna maji ya mvua

Spread the love

MATENKI 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu waziri wa Maji, Amos Makalla alipokuwaakijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inafikia hatua gani katika utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaondokana na tatizo la ukosefu wa maji.

Akijibu swali hilo, Makalla amesema  hadi sasa zaidi ya matenki 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika taasisi za shule na vituo vya afya.

Aidha, amesema  wizara imetoa maagizo kwa kila halmashauri kuwa na sheria ndogondogo zenye kuzilazimisha taasisi za serikali na watu binafsi kuweka miundombinu ya uvunaji maji kwenye majengo yao.

Amesema  katika utekelezaji huo, tayari halmashauri 11 zimekwishatunga sheria ndogo ndogo za uvunaji maji ya mvua.

Amesema  halmashauri 18 zinaendelea na taratibu za kukamilisha sheria hizo.

error: Content is protected !!