Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Matapeli waliotumia jina la Mke wa Magufuli kizimbani, wakosa dhamana
Habari Mchanganyiko

Matapeli waliotumia jina la Mke wa Magufuli kizimbani, wakosa dhamana

Spread the love

WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutumia jina la Mke wa Rais, John Magufuli, Janneth Magufuli kutapeli watu. Anaripoti  Faki Sosi … (endelea).

Watu hao ni pamoja na Saada Uledi, Maftaha, Heshima Ali na Shamba Ali ambao walitumia jina hilo kwenye mtandao wa Facebook kama taasisi ya Janneth Magufuli inayotoa mikopo kwa sharti la kutoa hela kama kinga ya mkopo huo.

Leo tarehe 18 Aprili  2019 Mbele ya  Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, wakili wa Serikali Batilda Mushi akisaidiana na Costanine Kakula wamewasomea washtakiwa mashtaka manne.

Shitaka la kwanza ni kula njama ya kutenda kosa ambalo linawahusu watuhumiwa wote. Wanadaiwa kuwa tarehe tofauti Januari mwaka 2017 na Machi 2019 watu hao walitenda kosa la kulanjama ya kuchapisha taarifa za uongo.

Shitaka la pili ni kuchapisha mapachapisho ya uongo  linawakabili watuhumiwa wote  ambapo inadaiwa walitenda siku tofauti  kati ya Januari mwaka 2017 na Machi 2019 ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Watuhumiwa walichapisha kuwa Janneth Magufuli ameunda Taasisi ya inayokopesha watu kwa sharti la kuwataka wakopeshwaji watoe hela kama kinga ya mikopo yao ilhali ni uongo.

Shitaka  tatu ni kujipatia fedha kwa njia ya ulaghai watuhumiwa wote wanakabiliwa na shitaka hilo. Inadaiwa walitenda kosa hilo kati ya tarehe 2 Machi 2019 na tarehe 8 Machi 2019 ambapo wakiwa kama waendeshaji wa akaunti ya Facebook yenye jina la Janneth Magufuli walijipatia kiasi cha Sh. 4.4 milioni kwa njia za ulaghai.

Shitaka la nne ni utakatishaji Fedha watuhumiwa wanadaiwa  kwa nyakati tofauti kati ya tarehe Januari 2017 na Machi 2019 walifanya utakatishaji  kiasi cha Sh4.4 Milioni wakijua kuwa nia zao haramu la ulaghai.

Wakili Batilda amedai kuwa upelelezi haujakamilika mpaka tarehe ya kutajwa. Hakimu Kasonde ameahilisha kesi hiyo mpaka  Tarehe 2 Mei 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!