Saturday , 4 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mataifa ya Magharibi kupeleka ndege za kivita Ukraine
Kimataifa

Mataifa ya Magharibi kupeleka ndege za kivita Ukraine

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Liz Truss amesema kwamba Uingereza na mataifa mengine yenye nguvu ya Magharibi yabap0aswa kutoa ndege za kivita kwa Ukraine kama sehemu ya msaada wa kijeshi wa muda mrefu. Anaripoti Rhoda Kanuti na misaada ya mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imekuja katika hotuba yake, aliyoitoa London, Truss amesema kuwa nchi za Magharibi zinapaswa kuwa tayari kutoa msaada kwa nchi hiyo.

Hata hivyo, Ukraine imekua ikiomba mara kwa mara ndege za kivita ,hasa wapiganaji wa zama za Usovieti ambazo marubani wao wanazifahamu.Washirika wa nchi za Magharibi wamesita kuchukua hatua hiyo kwa hofu ya kuichokoza Urusi.

Wakati wanachama wa Nato wakiongeza uungaji mkono kwa Ukraine, kwa silaha za masafa marefu, Truss amesema wanapaswa kwenda mbali zaidi.

Hatima ya Ukraine, inasema kwamba, ‘’inabakimkwenye usawa.’’Mataifa ya Magharibi yanapaswa kuwa tayari kuunga mkono Ukraine ,wakichimba kwa kina katika orodha zao ili kuipa nchi silaha nzito,vifaru na ndege.

Aidha amehimiza nchi za Magharibi kukataa uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Urusi,katika hotuba hiyo, Truss ametoa wito wa kuanzisha upya kwa mfumo wa kimataifa wa usalama ambao haukufaulu Ukraine.

Mataifa yenye nguvu ya Magharibi yanapaswa kukabiliana na uvamizi ,badala ya kutumia matumizi makubwa ya ulinzi ,utegemezi mdogo wa kiuchumi na miungano iliyoimarishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love  MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka...

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

error: Content is protected !!