June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Master Card yaweka wazi mikakati ya ushindi

Spread the love

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama ‘Scaling Competition’ ili kuongeza na kuimarisha upatikanaji wa fedha vijijini Tanzania, anaandika Aisha Amran.

Rai hiyo imetolewa na Gabriel Kivuti, mtaalam na mshauri wa Master Card Foundation leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji kwa wakulima wadogo wa barani Afrika.

Amesema taasisi yao inafanya kazi na mashirika yenye maono ili kufanikisha upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi maisha duni barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha kwa lengo la kupunguza umasikini.

Kivuti amesema kaya nyingi za vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za familia kusini mwa jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huo huo watoa huduma za kifedha wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika kufikia jamii, hivyo taasisi hiyo ikaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.

Ametaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo ni pamoja na vikundi vya akiba,bima ndogo ndogo na mifrumo ya umoja fedha, fomu za maombi za mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org.

Amesema jumla ya dola za kimarekani 10.6 milioni zimetolewa kwa washindi wa mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equit kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda, kwa kupitia kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaishi maeneo ya vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020.

error: Content is protected !!