January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mastaa wamlilia mama yake Lulu Diva

Lulu Abasi 'Lulu Diva'

Spread the love

 

MSANII wa Bongo fleva na muigizaji katika tamthilia ya jua kali, Lulu Abasi maarufu kama Lulu Diva amepata msiba wa kuondokewa na mama yake mzazi jana jioni tarehe19, Disemba 2021.  Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Lulu ambaye amekuwa akimuuguza mama yake kwa muda mrefu, alitumia nafasi yake kwenye jamii kuonyesha upendo kwa mama yake huyo na mara kadhaa alikuwa akimuweka kwenye ukurasa wake wa instagram.

Msanii huyo alienda mbali zaidi na kumtungia wimbo mama yake uliokwenda kwa jina la mama na hata kufanya naye video ya ngoma hiyo.

Aidha, kufuatia msiba huo, watu maarufu mbalimbali wameonesha kuguswa na msiba huo na kushare picha za Lulu Diva na mama yake na salamu za pole zinazoonyesha simanzi ndani yao,

Baadhi ya mastaa ambao walitoa salamu za pole kupitia mtandao wa Instagram kwenda kwa Lulu Diva ni pamoja na Diamond platnumz, Wema Sepetu, Rosa ree na Mimi mars.

Wengine ni Dogo janja, Nandy, lavalava, Esmaplatnumz, Jacqline Wolper, shilole, Faiza ally, Lilommy, Zamaradi Mketema, Linah sanga huku wengine wakiandika ujumbe wa pole kwenda kwa msanii huyo.

Msanii Nandy yeye ameandika “Pole lulu Mungu akupe nguvu wewe na familia nzima  R.I.P mama @luludivatz.

Diamond platnumz ameandika “ stay strong Divana”

Rosa ree, ameandika “Lulu jamani dahh sijui nisemeje  @luludivatz Mungu akufanyie wepesi na amlaze mama mahala pema peponi  r.i.p mamalulu

Huku msanii Wema Sepetu ambaye pia ni rafiki wa karibu wa msanii huyo ameweka taarifa za ratiba ya maziko itakavyokuwa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo ni kwamba baada ya dua itafanyika nyumbani kwa Lulu Diva, Mbezi beach Dar es salaam leo tarehe 20 Disemba, 2021 kuanzia saa saba mchana hadi saa tisa.

Mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Tanga – (Mafele) wilaya ya Muheza saa kumi jioni na mazishi yatafanyika kesho saa saba mchana.

error: Content is protected !!