March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Masogange ana kesi ya kujibu Kisutu

Agnes Masogange akiwasili mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema msanii wa filamu nchini, Aggnes Masogange ana kesi ya kujibu kwenye mashtaka yake ya matumizi ya dawa za kulevya, anaandika Faki Sosi.

Leo Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo baada ya upande wa Jamhuri kumaliza kuwasilisha ushahidi wake mahakamani hapo.

Ushahidi huo ulitolewa na askari wa Jeshi la Polisi, Sospiter kutoka ofisi ya upelelezi ya kituo kikuu cha Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Sospiter alidai mahakamani hapo kuwa baada ya kumpekuwa mtuhumiwa Masogonge alimkabidhi askari wa kike (WP), Judicy na kwenda naye kwa mkemia kwa ajili ya kupimwa mkojo.

Hakimu Mashauri alimuuliza mtuhumiwa baada ya kumkuta na hatia kwamba ni kwa namna gani atajitetea mahakamani hapo kati ya njia tatu ya kuwasilisha kiapo, kuleta mashahidi au kukaa kimya.

Mtuhumiwa Masogange aliomba kuleta kiapo na kuleta mashahidi watatu mahakamani hapo.
Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12 mwaka huu.

error: Content is protected !!