December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Masista 12 wafariki ndani ya siku 30

Spread the love

MASISTA 12 katika Mji wa Michigan, Marekani wamepoteza maisha ndani ya siku 30 (Mei 2020), kwa ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Mtandano wa CNN umeripoti…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao huo, masista wote hao walikuwa wajumbe wa Misheni ya Felician Livonia. Masista hao walikuwa na umri wa kuanzia miaka 69 hadi 99.

Masista hao ni Thoms Marie Wadowski (73), Mary Patricia Pyszynski (93), Mary Clarence (83), Rose Mary Wolak (86), Mary Janice (Margaret) Zolkowski (86), Mary alice Ann (Fernanda) Gradowski (73), Victor Marine Indyk (69), Mary Martinez (Virginia) Rozek (87) na Mary Madeline (Frances) Dolan (82).

Mkurugenzi Mkuu wa misheni hiyo Suzanne English, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo vilivyosababishwa na corona Jumanne wiki hii.

English amesema, masista hao wameacha historia yao iliyotukuka kwenye misheni hiyo tangu walipoanza kuitumikia kwa miaka tofauti katika maisha yao.

“Wametumikia maeneo mbalimbali kulingana na namna walivyopanda kuanzia kufundisha watoto mpaka kuwakinga na majanga,” amesema.

Amesema, miongoni mwa masista hao, mmoja wao alishinda tuzo ya uandishi wa mpango kazi wa biashara akishika nafasi ya pili na mwingine aliwahi kuitumikia Roma katika Ofisi ya Katibu.

“Tunaomboleza vifo vya masista ambao wamepoteza maisha kwenye kipindi hiki cha janga la corona, tunawashukuru wote waliowaombea wakati wa sala,” amesema Sista Mary Christopher Moore.

Masista wote hao walikuwa wakiishi kwenye kampasi ya 360 ambayo ni makazi ya masista 800. Masista walifariki baada ya masista hao 10 mpaka sasa (kuanzia Juni 2020) ni Mary Danatha Suchyta (98), Sister Mary Luiz Wawrzyniak (99), Sister Celine Marine Lesinski (92) na Mary Ester Printz (95).

error: Content is protected !!