MWIGULU Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi bado yupo kitandani katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma akitibiwa baada ya kupata ajali ya gari. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).
Ajali hiyo ilitokea jana 13 Februari 2019 katika eneo la Migori, Iringa mbunge huyo akirejea Singida kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya mkoa huo.
Akizungumza namna ajali ilivyotokea Mwigulu amesema, chanzo kikubwa ni dereva wake kukwepa punda watatu waliokuwa wakivuka barabara.
“Dereva wangu wakati anakwepa punda hao waliokuwa wakivuka barabara, alishindwa na baada ya hapo nilisikia kishindo kikubwa. Nilishtuma moshi ukiwa umetanda ndani ya gari ambapo tayari lilimuwa limepinduka,” amesema.
Mwigunu anasema, baada ya ajali hiyo, walitokeawasamaria wema waliomchukua na kumpeleka hospitali kupatiwa matibabu ambapo bado anayendelea na matibabu.
“Nashukuru Mungu naendelea na matibabu, baada ya ajali hilo walionileta hapa ni wasamaria wema,” amesema na kuongeza kuwa, mkanda ulimsaidia kwa kuwa ulikuwa umembana vizuri.
Leave a comment