Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Tangulizi Masikini! Mwandishi Kabendera apooza mguu
Tangulizi

Masikini! Mwandishi Kabendera apooza mguu

Mwandishi wa habari Erick Kabendera alipofikishwa mahamakani Kisutu leo
Spread the love

ERICK Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi ndani nje ya nchi, amepatwa na tatizo la kupooza mguu akiwa gerezani. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Taarifa ya wakili wake Jebra Kambole leo tarehe 30 Agosti 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeeleza, mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuhujumu uchumi, amepooza mguu na kuishia nguvu.

Mwandishi Kabendera alifikishwa mahakamani hapo tarehe 5 Agosti 2019, akikabiliwa na mashtaka matatu; kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.

Makosa hayo anatuhumiwa kuyatenda kwa siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam.

Katika tuhuma hizo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi mpaka ipate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP).

Kutokana na hali yake (Kabendera), Wakili Kambole ameiomba mahakama hiyo kulielekeza Jeshi la Magereza kumpeleka mteja wake kupata vipimo katika hospitali ya serikali.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega, Wakili Kambole amesema, alimtembelea mteja wake na kumkuta akiwa mgonjwa ikiwa ni pamoja na kushindwa kupumua vizuri.

“Nilipokwenda kumuona, nilikuta amepooza mguu na kushindwa kutembea, pia alikuwa akiishiwa nguvu. Hatujui nini kinamsumbua,” Wakili Kambole ameieleza mahakama.

Wakili wa Jamhuri Wankyo Saimon ameeleza, kuhusu maradhi hakuna anayeweza kupinga nalo, na kwamba haiwezekani Jeshi la Magereza likaelekezwa hospitali ipi mtuhumiwa anapaswa kupelekwa kupimwa.

Akisisitiza hilo Wakili Ankyo ameeleza, mtuhumiwa hajawahi kupeleka maombi ya kisheria akakataliwa, na kwamba kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi, hivyo Mahakam ya Kisutu haiwezi kufanya uamuzi wowote isipokuwa Mahakama Kuu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hadi tarehe 12 Septemba 2019 ambapo itarejeshwa kwa Hakimu Agustino Rwizile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!