August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Masikini Lema

Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini akiwa hospitali baada ya kuugua ghafla na kushindwa kufika mahakamani

Spread the love

KUZOROTA kwa afya ya Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini kumeingiza kiwewe kwa wakazi wa Jiji la Arusha na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika Wolfram Mwalongo.

Mbunge huyo ameshindwa kufika mahakamani jana kufuatia taarifa za kuugua ghafla akiwa mahabusu.

Sababu ya kudhoofu kwa afya ya Lema inadaiwa kwamba, tarehe 16 mwezi huu akiwa mahakamani hapo, aliomba ruhusa ya kumeza dawa kwa askari magereza mmoja aliyevalia mavazi ya kiraia, lakini hakupewa.

Wakili wa Lema (Sheki Mfinanga) mbele ya Agustino Rwezile, Hakimu Mkazi Mfawidhi anayesikiliza mashauri hayo ya jinai namba 351 na 352 ya mwaka 2016.

“Mheshimiwa Hakimu, mteja wetu (Lema) alipokuwa mahakama kuu aliomba maji kwa ajili ya kunywa dawa, askari magereza wakamnyima, afya yake inazidi kudhoofika na leo afya yake imezidi kuwa mbaya hajaweza kuletwa mahakamani,” alisema wakili wa Sheki.

Hata hivyo, hakimu Rwezile aliwataka mawakili wa serikali kueleza alipo mshtakiwa (Lema) kwa madai kwamba, wao ndio wenye jukumu la kueleza sababu kutofika mahakamani kwa kuwa yupo mahabusu katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo.

Kutokana na hali hiyo Mahakama hiyo imeahirisha mashauri hayo mawili ya jinai hadi Januari 18 mwakani.

error: Content is protected !!