March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Masikini Abdul Nondo!

Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP)

Spread the love

MAHAKAMA ya Mkoa wa Iringa imemkuta na kesi ya kujibu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Abdul Nondo aliyeshitakiwa kwa madai ya kusambaza taarifa za uongo kwamba ametekwa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 27 Agosti 2018, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Liad Chamshama ametoa uamuzi huo kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri. Hakimu amemtaka Nondo andae utetezi wake.

Hakimu Chamshama amesema kuwa, kutokana na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri mahakama hiyo imemtaka Nondo kujibu tuhuma hizo.

Nondo ameshitakiwa mahakamani hapo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kupita mtandao wa WhatsApp na kumdanganya Ofisa wa Polisi kwenye Kituo cha Polisi cha Mafinga.

Nondo alidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 7 Machi mwaka huu akiwa eneo la Ubungo Jiji Dar es Salaam na Mafinga mkoani Iringa.

error: Content is protected !!