December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Masikini Abdul! apigwa risasi ya kichwa, yupo taaban

Spread the love

IJUMAA ya tarehe 12 Julai 2019, imebaki katika kumbukumbu hasi kwa wakazi wa Kijiji cha Kufr Qaddoum kilichopo Kaskazini mwa Mji wa West Bank. Inaripotiwa kimataifa…(endelea).

Ni baada ya kushuhudia unyama aliotendewa Abdul Rahman (10), aliyepigwa risasi ya kichwa na wanajeshi wa Israeli kijijini kwaoQaddoum.

Siku ya tukio, Abdul alikua nyumbani pamoja na familia yao akicheza ‘game’ aina ya PUBG kwenye simu, ilikuwa kabla ya chakula cha mchana.

Abdul alitoka nje kwenda kucheza na wenzake. Saa nane mchana, Abdul alianguka chini baada ya mlio wa risasi, tayari alikuwa amepigwa risasi ya kichwa na mwanajeshi wa Israel. Haraka haraka alibebwa na kupelekwa hospitali.

Kwa mujibu wa ushuhuda wa tukiok, Abdul alipigwa risasi akiwa takribani meta 300 kutoka nyumbani kwao, mbali na eneo ambalo wanakijiji walikua wakifanya maandamano.

Kufr Qaddoum ni moja ya vijiji vya Wapalestina Kaskazini mwa Mji wa West Bank, ambao wakazi wake hutoka kila Ijumaa kuandamana na kupinga kitendo cha Israel kufunga barabara kuu kwa zaidi ya miaka 30 sasa, baada ya kujenga makazi ya Wayahudi kwenye ardhi yao kijijini humo.

Akitoa ushuhuda kuhusu tukio hilo Riyad Ishtaiwi, mkazi wa kijiji icho ambaye pia ni miongoni mwa watu wa mwisho kumuona Abdul ya kupigwa risasi, amesema kijana huyo alikuwa akicheza.

Mashuhuda walisimulia kuwa, damu nyingi ilimtoka Abdul na hivyo basi, alibebwa na kuwahishwa hospitali mjini Nablus kwa ajili ya matibabu.

Madaktari waliomtibu Abdul wamesema kwamba, risasi hiyo ilipasuka ndani ya kichwa na kutengeneza vipande karibu 100 ndani ya kichwa chake.

Istaiwi amesema kwamba, kitendo hicho kimesababisha huzuni na simanzi kubwa kijijini humo na kuwa, yeye (Istaiwi) alikuwa mwenye umri wa miaka 10 wakati Israeli ikipokonya Wapalestina ardhi katika kijiji hicho na kujenga makazi na kisha kufunga barabara.

Mashhour Qaddoumi, mkuu wa harakati za Fatah katika kijiji hicho alisema kwamba, kitendo hicho cha kupigwa risasi Abdul kilishtua kila mtu kijijini humo.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya wakazi wa kijiji hicho waliojeruhiwa tangu maandamano hayo ya wiki kuanza, alijibu, “swali linapaswa kuwa: ni nani ambaye hajawahi kujeruhiwa?”

Hata hivyo, Qaddoumi amesema kwamba, wakazi wa Kufr Qaddoum wataendelea kudai haki yao na kupigania haki na ardhi yao.

Dk. Othman Bisharat katika Hospitali ya Serikali ya Rafidya, Nablus alikolazwa Abdul amesema kwamba, hali ya kijana huyo ni mbaya  kwasababu risasi ilikuwa imepita nyuma ya ubongo.

Amesema, yeye mwenyewe alihesabu kati ya vipande 60 hadi 70 kwenye ubongo wa Abdul.

error: Content is protected !!