August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashishanga: Puuzeni mafisadi

Spread the love

STEVEN Mashishanga, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mstaafu amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupuuza mafisadi wanaotaka kuwagawa ili wasiunge mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli, anaandika Christina Haule.

 Mashishanga amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Waandishi wa Habari (Moro PC)  mjini humo.

Mashishanga ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Morogoro amesema, lengo la Rais Magufuli ni kutaka kuwahudumia wananchi kwa kuwaletea maendeleo na kuwafanya wawe na maisha bora.

“Umoja wetu Wana-CCM tusikubali kamwe ukagawanya na watu hao wasiopenda maendeleo, wala rushwa na mafisadi’’ amesema.
hata hivyo ameitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa mifugo iliyozidi katika mkoa huo kufanikisha azma ya mkoa kuwa Ghala la Taifa la chakula.

 

error: Content is protected !!