Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Mashine za kupimia wingi damu changamoto Mwanza
Afya

Mashine za kupimia wingi damu changamoto Mwanza

Spread the love

IMEELEZWA kuwa baadhi ya vituo vya afya mkoa wa Mwanza vinakabiliwa na ukosefu wa mashine za kupimia wingi wa damu kwa kinamama wajawazito pindi wanapokwenda kwenye vituo hivyo. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea). 

Hali hiyo imebainika baada ya uchambuzi uliofanywa na Amref katika kipindi cha Aprili – Juni 2018 kutoka kwenye mfumo wa taarifa za afya DHIS2 kwenye vituo vya afya 20.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa mradi wa Amref Health Africa, David Shayo wakati wa makabidhiano ya mashine za kupimia wingi wa damu kwa kinamama wajawazito katika mkoa wa Mwanza. 

Shayo alisema kuwa akinamama 5, 243 sawa na asilimia 34.5 kati ya 15, 197 ndiyo waliopimwa kutokana na uhaba wa mashine za kupimia wingi wa damu na wakati mwingine hutegemeana na mashine maabara ambayo hutoa huduma kwa wagonjwa wengine.

Alisema kutokana na hilo, Amref kwa kushirikiana na idara ya afya mkoa pamoja na halmashauri zinazotekeleza mradi liliamua kuanza kuboresha eneo hilo kwa kutoa mafunzo rejea kwa watumishi 60 kutoka vituo 20 vya kutolea huduma za afya.

“Mashine hizi zitatumika katika kitengo cha mama na mtoto na hii itasaidia zaidi kusogeza huduma karibu na kuondoa msongamano kwenye maabara za vituo vyetu na kumuhakikishia mama mjamzito kupata huduma zote eneo moja,” alisema Shayo.

Pamoja na hayo, alisema Amref kwa kushirikiana na  wizara ya afya, inatekeleza programu ya lishe inayofahamika kama Right Start Initiative Programu inayolenga kuboresha huduma za lishe kwa kina mama wajawazito, watoto wachanga, watoto wadogo chini ya miaka miwili na wasichana wa rika balehe.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Silas Wambura alisema msaada huo walioupokea utasaidia kwa kiasi kikubwa kupima wakina mama pamoja na watoto chini ya miaka mitano walipokuwa wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema Serikali inatambua mchango wa Amref katika suala la afya na kwamba serikali ya mkoa huo itaendelea kushirikiana nao muda wowote pindi wanapohitaji msaada wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaMakala & Uchambuzi

Uongo, uzushi, tiba ya matende, ngiri maji

Spread the loveKUNA uongo na uzushi katika jamii kuhusu wanaume, wanawake na...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Afya

Kambi ya matibabu ya kibingwa Ruangwa yaacha vilio, DC atoa ombi JAI

Spread the loveMKUU wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma amefunga rasmi kambi...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

error: Content is protected !!