Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Mashine za kisasa upimaji ardhi zaletwa
Habari Mchanganyiko

Mashine za kisasa upimaji ardhi zaletwa

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya upimaji ardhi jijini Dodoma ya Landnetwork (katikati) Samweli Ikwabe akionysha moja ya mashine ya kisasa ya upimaji ardhi jana Jijini Dodoma
Spread the love

KAMPUNI ya Land Network Ltd ya jijini Dodoma, kwa kushirikiana na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya upimaji ardhi Kolida ya nchini China, wameleta mashine za kisasa ambazo zitasadia kutatua changamoto ya ardhi nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jiji humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Land Network Ltd, Samwel Ikwabe amesema, mashine hizo walizoingiza nchini, zitasaidia kufanya upimaji wa Jiji la Dodoma kwa haraka na maeneo mengine nchini na kwa gharama nafuu.

Amesema, kutokana na uwezo wa mashine hizo ambazo zinasambazwa dunia kote na Kampuni ya Kolida ya China, wakazi wa Dodoma na maeneo mengine wanatakiwa kuchangamukia fursa hiyo ya kupimiwa ili waweze kumiliki ardhi.

“Maeneo mengi bado hayajapimwa hivyo kuwa moja ya sehemu ya migogoro ya ardhi, lakini pia wananchi wanaomiliki mashamba au ardhi kwa ujumla, hawana faidi nazo kutokana na kutopimwa.

“Hivyo kupitia mashine hizo, watapata fursa ya kupimiwa na kuweza kurasimishiwa makazi na kupata hati ya maeneo yao kwa gharama nafuu,” amesema Ikwabe.

Amesema, mashine hizo wanaweza kuzikodisha na kuziuza kwa wapimaji ardhi binafsi au wale wa halmshauri ambao wanachangamoto ya vifaa vya upimaji ardhi katika maeneo yao.

“Kupitia mashine hizi, kila mtu Dodoma atakuwa na uwezo wa kupimia kipande cha ardhi yake ili kiwe na tija kwa haraka na kwa bei nafuu,” amesema.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo Willson Waitara amesema kuwa, mashine hizo zilizoletwa kwa ajili ya upimaji ardhi kwa gharama nafuu.

“Kampuni hii ya kichina ni ya muda mrefu ambayo imeanzishwa toka mwaka 1989, ni takribani miaka 30 sas,a hivyo hawa wenzetu teknoljia yao ipo juu hivyo basi vijana wetu watapata fursa ya kujifunsa na kupata ujuzi katika mashine hizi,” amesema.

Mkurugenzi wa masoko wa kimataifa wa Kampuni ya Kolida, Andy Lau kutoka nchini China amesema kuwa, mashine hizo zimetengenezwa katika ubora wa hali ya juu ambazo zitasaidia katika kupimia ardhi kubwa kwa muda mfupi na kwa ubora zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!