June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashine za hospitali zimechoka-Kebwe

Mashine ya x-ray

Spread the love

SERIKALI imesema mashine za X-ray na Ultrasound zinazotumika katika hospitali za wilaya mbalimbali hapa nchini ikiwemo ya Babati, huaribika kutokana na uchakavu wake. Anaadika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Stephen, ameliambia Bunge wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum Pauline Gekul (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali inatumia wakala mmoja “Philips” katika kutengeneza mashine za x-ray na Ultrasound ambazo huaribika mara kwa mara.

Pia alitaka kujua ni kwanini mashine hizo uharibika mara kwa mara hapa pele zinapokuwa zimetengenezwa kwa muda mfupi.

Dk.Kabwe alisema serikali imekuwa ikitumia walaka huyo Philips kwa kuwa ndiye mtengenezaji, msambazaji na kupitia taratibu za manunuzi ndiye anayefanya matengenezo na kwamba hospitali za wilaya, mikoa, kanda na taifa mashine hizo pia ni Philips.

Amesema mashine hizo kuharibika kila mara kutokana na uchovu kwa kuwa zimeendelea kutumika toka mwaka 1999 hadi sasa ambapo ni takribani miaka 16 sasa.

“Kwa sasa, serikali ina mpango mkakati wa kuzibadili mashine hizo moja baada ya nyingine na tayari mashine 4 za x-ray na Ultrasound 14 mpya zipo bandarini na zonasubiri utaratibu wa ugomboaji.

“Serikali kupitia wizara za Afya na Ustawi na Jamii, Fedha na Uchukuzi zimekamilisha utaratibu wa mashine zilizopo bandarini na vipuri vilivyopo uwanja wa ndege ili wakati wowote vipelekwe katika hospitali husika,” amesema Dk.Kabwe.

error: Content is protected !!