October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashine ya kupima corona yatua Zanzibar

Aliyekuwa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Spread the love

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imepokea mashine moja kati ya tatu ya kupima ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa, tarehe 15 Mei, 2020 na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zanzibar, Dk. Juma Mohammed Salum imesema mashine zingine mbili zinatarajiwa kufika wakati wowote na zitafungwa Ugunjwa na Pemba.

“Mashine ilityowasili inatoka Korea Kusini kwa ufadhili wa (SMZ) na mfanyabiashara maarufu Tanzania, Rostam Aziz,” amesema Dk. Salum

Mkurugenzi huyo amesema, mashine hiyo inauwezo wa kutoa majibu ndani ya masaa manane kwa vipimo vya watu 96, hivyo kwa saa 24 inauwezo wa kutoa majibu ya vipimo 288.

Tarehe 25 Machi, 2020, Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein alifanya ziara kuangalia ujenzi wa maabara ya uchunguzi ya Microbiology katika Kijiji cha Binguni na kuagiza wizara ya afya kuanza mara moja ujenzi wa maabara itakayochunguza maradhi yanayosababishwa na virusi (Virology Labaratory).

Katika maagizo yake, Rais Shein alisema wizara hiyo inapaswa kuhakikisha ujenzi wa maabara hiyo unakamilika haraka iwezekanavyo ili Zanzibar iweze kuwa na mashine zake za kupima corona.

Kabla ya mashine hiyo, Zanzibar ilikuwa ipima sampuli zake katika maabara iliyopo Tanzania bara ambayo hata hivyo, kwa sasa imesimama ikifanyiwa maboresho yaliyoelezwa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya kwamba mara baada ya kumalika wataanza kutoa taarifa.

Hadi leo Ijumaa, Tanzania imeripoti wagonjwa wa corona 509 kati yao 183 wamepona huku vifo vikiwa 21.

error: Content is protected !!